Kama ni hivyo kwanini CCM wananajisi uchaguzi chini ya Magufuli ili waendelee kubaki madarakani? Kwanini wasiheshimu matakwa ya wananchi ili wapishe watanzania wengine nao watawale? Hiyo katiba bora kikwazo ni hao ccm, huku Magufuli unayemkubali akiwa kikwazo namba moja wa katiba bora.
Ni Hadi tutakapo pata utaratibu wa kuwafunga viongozi wakitoka madarakani kama walivo wenzetu ndio tutakuwa na maendeleo,Kinga ya kutoshtakiwa tutasubiri Sana huku tukiendelea kuvuna mabua miaka 60 ya Uhuru bado tunavuna mabua tu.Wasalaam wana JF!
MOLA tuepushe na janga la Corona Amina.
Kuna watu huwa wanasema wakiwataja baadhi ya wanasiasa hususani wapinzani, kwamba watukomboe dhidi ya utawala uliopo wakimaanisha CCM.
Huwa najuliuliza huwa wanamaanisha kitu gani hasa? Kwa kuwa wanaotawala ni Watanzania wenzetu, wenye familia na mfumo wa maisha kawaida kabisa na sisi.
WanaCCM, WanaCHADEMA, wana CUF, ACT na vyama vyote, wote ni Watanzania wenye akili tofauti, imani tofauti, mitazamo tofauti, chama chochote kinachopata nafasi kutuwala kitawatumia watanzania hawahawa katika administration yake.
Hakuna chama kitakuja na brand ya Watanzania tofauti na sisi tuliopo, kitatawala na hawahawa tuliopo.
Wezi watakuwepo, mafisadi watakuwepo, waadilifu watakuwepo pia.
Binafsi sioni chama ambacho mtu atanishawishi kusema eti kitaleta ukumbozi, ni uongo!
USHAURI WANGU:
Ikiwa tutakuwa na KATIBA ambayo itaweka malengo ya Tanzania mbele kwamba chama chochote kitakacho tawala, basi kielekeze katika malengo MAMA.
Tusitegemee ILANI ZA VYAMA pekee, So kama taifa tufikiri katika kuboresha katiba YETU.
Tujiwekee malengo ya muda mrefu kama taifa, KATIBA bora ndio dili kwa mtazamo wangu.
JITAHIDI KUWA MWAMINIFU KWA NAFASI YEYOTE UNAYOPATA KUTUMIKA, SIKU MOJA UTATOA HESABU KWA MUNGU. USILAUMU MTU, WEWE KATIKA NAFASI ULIOPO NI MWAMINIFU KIASI GANI?
KILA MMOJA WETU AKIWA MWAMINIFU TUTALIJENGA TAIFA LETU PAMOJA
Hata hivyo naukubali utendaji wa mh John P. Magufuli.
Ni hayo tu....
Sent using Jamii Forums mobile app
Inawabana watawala inawwazuia kuwa mungu watu.Tuendelee tu kuombea kizazi cha zamani kizidi pungua tupate kizazi kipya chenye global vision cha kuwawajibisha na kuwashughulikia watawala waendao kinyume na katibaKugusia mchakato wa katiba mpya awamu hii hlo swala ni kama halipo na cjajua kuna siri gani nyuma ya hii delay
Kwa katiba hii chakavu still wakiingia wengine wasio wa upande wao watalimia meno.Mfumo wetu mfumo ukishakutupa huna chako unaweza fanywa chochote na waliopo Sasa kama ulitupa mawe kwenye vioo vya wenzako jiandae nawe kutupiwaMkuu kulikuwa na rasimu ya Warioba, wananchi walitoa maoni yao, lakini ccm kwa wingi wao wakachakachua maoni ya wananchi. Basi haidhuru hiyo rasimu ilichakachuliwa, kulikuwa na katiba pendekezwa iliyokuwa imefikia hatua ya kura za maoni, lakini hata hiyo Magufuli aliikataa. Sasa naona unamkubali mtu asiyetaka katiba bora, bali anataka hii hii ili ubovu uendelee. Kwa maneno marahisi unataka CCM iendelee kukaa madarakani, maana unadhani wengine wote watakaokuja watakuwa kama hawa CCM uliowazoea.
Ni Hadi tutakapo pata utaratibu wa kuwafunga viongozi wakitoka madarakani kama walivo wenzetu ndio tutakuwa na maendeleo,Kinga ya kutoshtakiwa tutasubiri Sana huku tukiendelea kuvuna mabua miaka 60 ya Uhuru bado tunavuna mabua tu.
Mwafrika yeyeto usipomuwekea mfumo wa kumdhibiti hawezi kuwa na tija ni lzm ataumiza wenzake.Check South Africa, Zimbabwe,Congo nk mobutu,zuma,bokasa, mugabe walijijengea makasri mahekalu kwa wizi wa Kodi za umma utadhani awatokufa.Lkn huwezi sikia watawala wa kikoloni mfano kina Ian Smith,Pita Botha,de Clark waliiba Kodi za umma wakajimilikisha na kujenga mahekalu popote duniani,isipokuwa hawa wakoloni weusi ni Sababu hawana mfumo wa kuwabana katiba zinawaruhusu kufanya chochote wajisikiacho kuuwa,kuiba,kuuwa uchumi, kuleta umasikini,nk huku wakipewa Kinga,hii iko Africa pekee thus hatuwezi endelea tofauti na wenzetu viongozi wao hawana room ya kuchezea katiba zao huwezi unakwenda jela wanaweka mwingine thus wanasonga.Wow, nimewahi kusema hiki kitendo cha rais kuwa juu ya katiba na kutoshitakiwa akiwa au ametoka madarakani, ndio chanzo halisi cha maovu yote ya kimfumo ndani ya nchi hii. Siku tutatakapotoa hicho kifungu, zile amri za nyuma ya pazia ziitwazo amri toka juu itakuwa ndiyo mwisho. Kwa sasa hivi amri toka juu ina nguvu kuliko katiba na sheria. Na kimsingi amri hii toka juu ndio inayoagiza mambo yote machafu hapa nchini, na mwanya huo hupatikana kupitia madaraka ya urais.
Mkuu kulikuwa na rasimu ya Warioba, wananchi walitoa maoni yao, lakini ccm kwa wingi wao wakachakachua maoni ya wananchi. Basi haidhuru hiyo rasimu ilichakachuliwa, kulikuwa na katiba pendekezwa iliyokuwa imefikia hatua ya kura za maoni, lakini hata hiyo Magufuli aliikataa. Sasa naona unamkubali mtu asiyetaka katiba bora, bali anataka hii hii ili ubovu uendelee. Kwa maneno marahisi unataka CCM iendelee kukaa madarakani, maana unadhani wengine wote watakaokuja watakuwa kama hawa CCM uliowazoea.
Kugusia mchakato wa katiba mpya awamu hii hlo swala ni kama halipo na cjajua kuna siri gani nyuma ya hii delay
Ni Hadi tutakapo pata utaratibu wa kuwafunga viongozi wakitoka madarakani kama walivo wenzetu ndio tutakuwa na maendeleo,Kinga ya kutoshtakiwa tutasubiri Sana huku tukiendelea kuvuna mabua miaka 60 ya Uhuru bado tunavuna mabua tu.
Inawabana watawala inawwazuia kuwa mungu watu.Tuendelee tu kuombea kizazi cha zamani kizidi pungua tupate kizazi kipya chenye global vision cha kuwawajibisha na kuwashughulikia watawala waendao kinyume na katiba
Usitudanganye wewe Ccm huwa inawakilisha aina flan ya watu walio kata tamaa kama ilivyo wewe na mawazo ya kizee zee
Ila vyama safi kamaa Act vina fikra ya ukombozi
Mwafrika yeyeto usipomuwekea mfumo wa kumdhibiti hawezi kuwa na tija ni lzm ataumiza wenzake.Check South Africa, Zimbabwe,Congo nk mobutu,zuma,bokasa, mugabe walijijengea makasri mahekalu kwa wizi wa Kodi za umma utadhani awatokufa.Lkn huwezi sikia watawala wa kikoloni mfano kina Ian Smith,Pita Botha,de Clark waliiba Kodi za umma wakajimilikisha na kujenga mahekalu popote duniani,isipokuwa hawa wakoloni weusi ni Sababu hawana mfumo wa kuwabana katiba zinawaruhusu kufanya chochote wajisikiacho kuuwa,kuiba,kuuwa uchumi, kuleta umasikini,nk huku wakipewa Kinga,hii iko Africa pekee thus hatuwezi endelea tofauti na wenzetu viongozi wao hawana room ya kuchezea katiba zao huwezi unakwenda jela wanaweka mwingine thus wanasonga.
Naamini mzee Magufuli nimuelewa, approach iwe nzuri tu. Ata take action I believe
Sent using Jamii Forums mobile app
Ila umeelewa hoja yake kuu?Kugusia mchakato wa katiba mpya awamu hii hlo swala ni kama halipo na cjajua kuna siri gani nyuma ya hii delay
Mkuu, watathimini hao wanaACT, halafu uniambie ni nani unamuwekea tumaini lako
Sent using Jamii Forums mobile app