Baadhi ya Watanzania wana roho mbaya sana. Kwanini hamripoti hali ngumu za watu?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
8,992
2,000
Baadhi ya Watanzania tena sio idadi ndogo ni watu ambao wamekosa busara, wenye husuda na roho mbaya sana wanaweza wakakuua bila kosa.

Maisha yanapokupiga hawana habari na wewe wala hawaendi TAKUKURU au kwenye vyombo vingine kupeleka habari kua fulani kapigika kimaisha.

Sasa kwanini mnashughulishwa na watu waliofanya juhudi zao na Mungu akaweka baraka kwenye kazi za mikono yao hadi mnapeleka taarifa za uongo ili wenzenu wapate matatizo? Umeibiwa chochote? Umedhulumiwa chochote na muhusika? Una mdai kitu gani muhusika hata kama ni shilingi moja tu upewe na riba ya aslimia elfu moja ili uache roho mbaya!!!?

Uzuri watumishi wa kwenye vyombo hivyo nao ni binadamu, wanaona na wanajua roho mbaya za watu na maonevu na wivu walikua nao baadhi ya watu juu ya Wananchi wenzao na wakati mwingine wakishajiridhisha kuwa umeonewa wanaweza wakakudokeza kilichotokea japo si maadili ya kazi zao na utashangaa aliyekusingizia!

Wee jamaa nimetukana kimoyomoyo matusi yote niyajuayo na mengi ni ya nguoni ila Mungu hawaruhusu waja wake wafanye wanavyotaka. Lakini sifichi natamani mabaya juu yako kwa sababu hujui njia zangu za wala mimi sijui na sina haja ya kujua zako kwa hiyo hukua na sababu zaidi ya wivu, husuda na roho mbaya kufanya uliyoyafanya.
 
Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
3,825
2,000
Pole sana mkuu, wahenga hawakukosea waliposema ni heri wali nyama kuliko walimwengu,
Wameshawekwa duniani tuishi nao hakuna namna ya kuwakwepa, ni ndugu zetu wa karibu, ni rafiki zetu wa karibu kabisa lakini kiuhalisia wengi wao ndiyo wabaya wetu.!!

Upo sahihi kuwa na hasira, ila haupo sahihi kumuombea mabaya, sasa ukimuombea mabaya wewe na yeye mnakuwa mna tofauti gani??
Nimejifunza kumuombea aliyeniumiza mema sababu najua kwa kufanya hivyo ninaonesha hasa upendo wa Kimungu na ninajua ukimuombea mtu mema, mema yatakurudia maradufu.!!

Learn to see positivity in every action, lisingetokea hilo pengine usingefahamu yeye ni mtu mbaya kwako kwa kiasi gani, nadhani ungeendelea kumuamini, ama pengine usingejifahamu wewe Sesten una uvumilivu kwa kiwango gani, Wakati mwingine tunapitishwa kwenye mabaya ili tujifunze lililo jema.!!

'Usimuamini mtu hata kama unamtania'..!!
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
8,992
2,000
Pole sana mkuu, wahenga hawakukosea waliposema ni heri wali nyama kuliko walimwengu,
Wameshawekwa duniani tuishi nao hakuna namna ya kuwakwepa, ni mdugu zetu wa karibu, ni rafiki zetu wa karibu kabisa lakini kiuhalisia wengi wao ndiyo wabaya wetu.!!

Upo sahihi kuwa na hasira, ila haupo sahihi kumuombea mabaya, sasa ukimuombea mabaya wewe na yeye mnakuwa mna tofauti gani??
Nimejifunza kumuombea aliyeniumiza mema sababu najua kwa kufanya hivyo ninaonesha hasa upendo wa Kimungu na ninajua ukimuombea mtu mema, mema yatakurudia maradufu.!!

Learn to see positivity in every action, lisingetokea hilo pengine usingefahamu yeye ni mtu mbaya kwako kwa kiasi gani, nadhani ungeendelea kumuamini, ama pengine usingejifahamu wewe Sesten una uvumilivu kwa kiwango gani, Wakati mwingine tunapitishwa kwenye mabaya ili tujifunze lililo jema.!!

'Usimuamini mtu hata kama unamtania'..!!
Asante sana dada kwa ushauri wako, kuna kitu umenifundisha na hakika nakiri nimekosea kumtakia mabaya. Nitajirekebisha kuanzia kwenye moyo na nafsi yangu
 
Ngorunde

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
1,922
2,000
Pole kwa machungu yaliyokukuta.

Ila punguza kulalamika, maana kwa jinsi ulivyoandika hata huyo unayetaka kumfikishia ujumbe sidhani kama atajijua. Umeandika mno kiujumla....hii ni sawa na umeudhiwa ukumbini ukaenda kulilia chooni.
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
8,992
2,000
Pole kwa machungu yaliyokukuta.

Ila punguza kulalamika, maana kwa jinsi ulivyoandika hata huyo unayetaka kumfikishia ujumbe sidhani kama atajijua. Umeandika mno kiujumla....hii ni sawa na umeudhiwa ukumbini ukaenda kulilia chooni.
Asante kwa ushauri mkuu wangu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom