Baadhi ya wanaume Mungu anawaona...

dadapesa

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
366
655
Habarini wana jf, natumaini mu wazima, niende moja kwa moja kwenye mada.

Nina Dada yangu wa hiari anapitia mazito saana ,mwenyewe ana dai hii ni zaidi ya mikosi. yeye ni mfanyabiashara tu mdogo amejiajiri anaendesha maisha yake yanaenda. iko hivi kipind cha nyuma alikuwa na mahusiano na MTU ambaye walipendana sana ,mwanaume huyo alikuwa nje ya mkoa wa dar hivo Dada akawa anaenda Mara moja moja kumtembelea mpenz wake Huyo aliyedumu nae kwa miaka miwili kwa kipind hicho.

Katika mahusiano yake alibahatika kupata ujauzito akaona sio shida sana kwa sababu umri uliruhusu basi wakapanga mipango wakajitambulishe , sasa mimba ikiwa na miez miwil mwanaume akawa haeleweki akakata mawasiliano ghafla bila sababu yoyote akipigiwa hapokei mwishoni akaja kubadilisha namba kabisa akawa hapatikani.

Alijitahidi kulea mimba mwenyewe but ilivyofika miez saba hiv alienda kumtafuta alimkuta katika mahojiano ya hapa na pale akasema ameamua tu iwe ivo anasubir mtoto akizaliwa atamlea mwanawe kumbe nyuma yake alikuwa na mwanamke mwingine ambaye naye alikuwa mjamzito na tayari alishamtambulisha nyumban kwao ( Dada ilibidi apeleleze ajue kwa nini Huyo mwanaume alimgeuka ghafla wakati hakuwahi kumkosea akaja kugundua hivo kuwa mwanaume alikuwa na mtu mwingine aliyempenda zaidi)

Mungu alimjaalia akajifungua vizur mtoto wake akawa anamlea mwenyewe pasipo msaada wa baba wala wa MTU yoyote maisha yakaenda. sasa kama binadamu huwez kukaa tu hivi hivi ikapita ka miaka mitatu hivi akajitokeza MTU mwingine aliyeonyesha kumpenda sana

Mwanaume huyo alikuja kwa gia zote na kujifanya mcha Mungu,akajifanya kumpenda mwanae na kumletea zawad zawad na ahad kama zote za kumsomesha, bas wakajikuta wanapendana sana wakatambulishana kila mahali ,mwanaume akawa anakuja kwa mwanamke Mara kwa mara coz Dada ye alikuw busy na kazi analala asubuh anaondoka.

Siku zimesonga mbele akajikuta anapata ujauzito ,hakuona kama kuna shida coz ni MTU anayejulikan bado tu vitu vidogo vidogo waweze kuishi kulea familia,.ukizingatia umri nao umeshaenda basi likawa jambo La furaha mwanzoni.

Mimba ikiwa na miezi miwili ama mitatu hivi yule kaka akasema anasafiri anaenda kwenye interview, wakakubaliana vizuri( hapo ikumbukwe mwanamke ye ndo alikuwa kila kitu coz mwanaume kwa wakati huo alikuwa hana kazi )

Migogoro ilianza alipoondoka , alikaa huko huko akiulizwa vipi majibu bado nafuatilia kazi. mawasiliano akakata na akawa kama MTU flan anakwepa kwepa hivi. jaman kuna vitu watu wanapitia unaeza sema labda ni kwa sababu labda hakuwa MTU aliyetulia na kuhangaikia mabwana si kweli kwa huyu MTU naemzungumzia hapa. akitoka ofisini ni nyumban direct siku zote za juma ndo ratiba yake. huyo kaka ye ndo alikuwa akimfta nyumban kwake.


Juzi nimeonana nae ameniambia mambo mengi sana mengine siwez hata kuyaelezea hapa mana sitamaliza. yule mwanaume ndo kashaingia mitini tena anajilaumu kama mimba ingekuwa ndogo angefanya abortion basii ila its too late. anahangaika mwenyewe.

Ushauri niliompa nilimwambia tu kwa kuwa wakanza alilea na akakua na huyo ajae atakuwa tu cha msingi asiingie tena kwenye mahusiano akae alee watoto wake basi mbona kuna wanawake wengi wanalea familia zao mwenyewe hawajaolew na wanamafanikio makubwa tu.


Kinachomtatiza hadi sasa ni kuhusu kumwandikisha mtoto ( kijacho) majina amemchukia sana huyo mwanaume hataki hata kumwandikisha mtoto huyo majina ya huyo baba ake aliyemtelekeza coz had sasa hawana mawasiliano yoyote, na wala hakuwahi kumpa huduma yoyote hadi sasa, nimemwambia nenda ustawi wa jamii ukalalamike akasema hawez kuwa na huo muda wa kuacha shughuli zake na kwenda kumshtaki mtu ye kama ameona ni sahihi kutelekeza ujauzito basi.

Kingine nilichomshauri nilimwambia basi aandike majina ya ukoo wake jambo alilolikataa kabisa coz hata yeye alitumia majina ya mzazi wake wa kufikia na mambo aliyomfanyia had anakuwa ni meengi na mabaya.

Ushauri wako ni muhimu sana, natanguliza shukran za dhati
 
Alee mtoto, majina si issue sana hata la mjomba wake litamfaa au babu yake.

Nyie wanawake:
Kutambulishwa kusiwe kutambulishwa tu, bali unatambulishwa kwa nani? (muhimu sana hili) kama unataka kujua utambulishwe kwa nani njoo DM.

Kubeba mimba kwa mihemko ya mapenzi ni kosa kubwa, kumbukeni wanaume tuna ile tamaa ambayo unaweza dhani ni mapenzi, kumbe mtu katamani mguu, tako, sauti au rangi.


Exclusive:
Nina kamchepuko kangu kanataka nikajaze mimba ,sema nakaonea huruma kwani naona kama hakajatambua nini kanahitaji maishani.
 
..wewe unadhani mwenye matatizo hapo ni nani?

Mama wawili, baba tofauti halafu single. Je, ni mzuri wa sura?
 
ni mzur mwenyewe afu anajipenda mi nashindwaga kuelewa hapo inakuaje mdada mzur vile hata kuolewa haolewi
 
Wanaume wanalaumiwa bure tu hapa. Obviously both guys hajui nyumbani kwao kwa wazazi wa hao majamaa thats why wakibadilisha number tu kawapoteza mazima. Wanakutana kimjini mjini tu wanakulana dada anakua comfortble anabeba mimba. Hapo wa kulaumiwa ni yeye kwani hajui kama kuna njia nyingi za uzazi wa mpango.

Hiyo pesa anayotumia kulea watoto wawili wasio na baba si angeinvest angekua mbali sana.

It's easier to blame other people for your misfortunes.
 
Wanaume wanalaumiwa bure tu hapa. Obviously both guys hajui nyumbani kwao kwa wazazi wa hao majamaa thats why wakibadilisha number tu kawapoteza mazima. Wanakutana kimjini mjini tu wanakulana dada anakua comfortble anabeba mimba. Hapo wa kulaumiwa ni yeye kwani hajui kama kuna njia nyingi za uzazi wa mpango.

Hiyo pesa anayotumia kulea watoto wawili wasio na baba si angeinvest angekua mbali sana.

It's easier to blame other people for your misfortunes.
niko chimbo napata moja baridi moja moto, comment yako imenifurahisha na kunielimisha hvyo naomba nikupongeze kwa savannah 3 tu.
 
Mkitangaziwa ndoa mnatoa mbunye kwa speed ya 4G ili muolewe,mtu hana kazi unadate nae na kumtunza kama mwanao
 
pole yake bt mkumbushe changamoto tumeumbiwa wanadamu hivo asiache kumshukuru mungu maana changamoto yake ni ndogo sana kuliko wanazopitia wengine.
 
Wanawake wafuate maadili, bila ya ndoa usifanye ngono. Baki mwenyewe kama itagharimu kutokuolewa.
Kama mtu hana mpango na yeye wala mtoto, unampa aje mtoto jina la mtu baki? Huyo rafiki yako inabidi ajitambue!
 
Back
Top Bottom