Baadhi ya viongozi Serikalini ni vibaka waliojivika vazi la uongozi

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,900
3,201
Habari za leo wana jamvi,

Moja kati ya vitu vya muhimu sana ili nchi iendelee, lazima uongozi uwe vizuri. Viongozi wawe waadilifu na watambue kwamba wapo kwenye nafasi walizopo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi kwa ujumla.

Bahati mbaya sana tuliyo nayo kama Taifa, ni ile hali ya viongozi wetu kujali zaidi maslahi yao, kuliko kujali maslahi ya Wananchi na nchi yote kwa ujumla. Kwa maneno ya kihuni wanaita kula urefu wa kamba (kama mbuzi), sasa shida ya baadhi ni walafi na hawatosheki hata wakiiba kiasi gani! Msisitizo uwe kwenye baadhi ya viongozi.

Kwa maneno hayo machache, nadiriki kabisa tena kwa kujiamini kwa asilimia zote, kusema kwamba baadhi ya viongozi wetu wa serikali katika nafasi mbalimbali, ni VIBAKA waliojivika tu vazi la Uongozi.

Ahsanteni sana.
 
Kwa hili Mh.Musukuma mwenyewe ni shahidi, naona wakati mwingine unakuwaga na vi-element vya uzalendo.
 

Attachments

  • MUSUKUMA_AWAWASHIA_MOTO_MAWAZIRI_NA_WEZI_WA_MALI_ZA_UMMA_MUDA_HUU_BUNGENI(144p).mp4
    14.4 MB
Huyu anafundisha jinsi ya kuiba na kutafuna hela za uma kwa stepu👇😁😁😁
 
Back
Top Bottom