Baadhi ya mambo yanayochangia kupata laana zisizotarajiwa

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Barabarani, unakutana na mwanamke mchuuzi masikini mwenye mtoto mgongoni, unashusha kioo cha gari lako na kumuuliza kwa sauti ya kijeshi:

"Unauza bei gani hivyo vitunguu na hizo ndizi?" Muuzaji masikini kwa upole anakujibu "shilingi elfu moja kwa kichane cha ndizi, na elfu moja kwa fungu la vitunguu." Kwa kiburi unamwambia unahitaji kichane cha ndizi kwa shilingi mia tano na fungu la vitunguu kwa shilingi mia tano, au vinginevyo haununui.

Muuzaji masikini anakubaliana na hali na kukujibu, "Chukua tu kwa bei unayotaka, sijauza chochote tangu asubuhi, walau sasa nipate cha kununulia watoto chakula cha usiku."

Amepata hasara, lakini zaidi anaenda kukununulia pia mfuko wa kuweka bidhaa hizi ulizo nunua. Unamwagiza afanye haraka vinginevyo utabadili mawazo. Anaomba msamaha, na kwa tabasamu anakukabidhi bidhaa zako, anakubariki pia kwa kumuungisha.

Unamrushia hela na kuchomoka kwa kasi na kumwachia wingu la vumbi na moshi linalomfunika yeye na mtoto. Anakohoa wakati anaweka vizuri fedha kidogo alizopata. Umaskini haujamwachia uchaguzi.

Umefika sasa kwenye hoteli ya nyota tano, ambapo utakutana na rafiki zako. Unawaambia waagize chakula na vinywaji kadiri wanavyotaka. Wanaagiza vyakula vya gharama kubwa, na mabaki ya chakula ni mengi kuliko chakula walichokula. Gharama nzima inakua shilingi laki tano. Unalipa bila kuomba upunguziwe, unampa mhudumu tip ya shiligi elfu kumi shukrani kwa chakula alichowahudumia ambacho hamkula hata nusu yake.

Tukio hili linaweza kuonekana la kawaida kabisa kwako, lakini sio la kibinadamu.

Point ni kwamba:-
Kwanini kila mara tunaonyesha tuna nguvu ya kubishania bei wakati tunaponunua kutoka kwa maskini?
Kwanini tunakua wakorofi tunaponunua kwa maskini?
Kwanini tunakua wachoyo tunaponunua kwa wahitaji?

Kwanini tunaonyesha ukarimu kwa wale ambao wala hawahitaji ukarimu wetu?
Kwanini tunaonyesha upole na utu tunaponunua kwa watu matajiri ambao wanaona hela yetu kama chenchi ndogo tu?
Kwanini tunaelekeza fedha zetu kwenye bahari ya fedha?

Tafadhali nunua vitu rahisi kwa watu maskini kwa bei ya haki
Wakati mwingine, makusudi lipa na ziada unaponunua kutoka kwa mwanamke au hata mwanaume masikni.,Hii inaweza kukupa baraka ambazo kibinaadam huwezi kujua kuwa kuwa Mungu amekurudishia pale ulipopunguza.
Mungu atujaalie moyo wa Upendo. Amina.
 
Ujumbe murua na wakati sahihi wa kutukumbusha, ili mwaka mpya watu wenye tabia hii wabadilike.
Mara nyingi wachuuzi wadogo wadogo, huwa wanatafuta hela ya kula siku hiyo na watoto wake.

Siku mojamoja jaribu tu kununua kwao hata kama wewe, huitaji hiko kitu. Utampa mwenye uhitaji, utakuwa umepiga ndege wawili kwa jiwe moja.
 
 
Ni sahihi lakini nao wauzaji wa barabaran wahuni Sana.

Laaana anatoa Nani na umasikini anatoa nani?
 
Hakuna laana ya hivyo,kwani ww ndio umemfanya awe masikini,tafuta hela
Usimuonee huruma mwanamke,usimuonee huruma masikini
Hawanaga huruma hao viumbe
Hawana dhukrani
Umasikini sio sifa,wapambane,hata wenye magari wengine sometime hawana kitu mfukoni wanaunga unga tu
 
Biashara ni makubaliano,kwani anakua kamlazimisha au kamnyang'anya.? Sisi wengine tutanunua hata Mia tatu Mia tatu
 
Afadhali ya hio mwingine kaambiwa na ndugu yake kua anashida na asimpekabisa ilaakifika kwa masela yy ndio mfadhili mkuu
 
Back
Top Bottom