Baadhi ya Mambo yaliyoanzishwa na Rais Benjamini Mkapa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,078
10,023
Benjamin William Mkapa alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995 na alikuwa madarakani kuanzia mwaka 1995 hadi 2005. Katika utawala wake alifanya mengi haya ni machache kati ya hayo.

TAKUKURU. Kabla ya kuwa TAKUKURU kwa sheria ya TAKUKURU ya 11 ya mwaka 2007, ilikuwa inafahamika kama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, TAKURU, ambayo ilianzishwa kwa sheria ya TAKURU ya 2002, kipindi ambacho Rais Mkapa alikuwa madarakani.

TASAF ni Mfuko wa maendeleo ya jamii ulionzishwa ukiwa na madhumuni ya kutoa fursa kwa kaya masikini kuongeza kipato ili kumudu matumizi ndani ya kaya. Mfuko huu ulianzishwa mwaka 2000 baada ya tafiti kufanyika mwaka 1999.

Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, NHIF. Mambo mengine ni pamoja na SUMATRA ambayo kwa sasa inaitwa LATRA. Pia EWURA, BRELA na TANROADS ni kati ya mambo yaliyoanzishwa katika utawala wa Mkapa.
 
Kabla ya TAKURU(PCB) ile ya Jenerali Kamazima mapambano ya Rushwa yalikua yanaongozwa na Kikosi Cha Kupambana na Rushwa(Task Force) iliyokua inahusisha Polisi na UWT

Ndio maana mpaka leo TAKUKURU hawana chuo bado mafunzo yao mengi wanachukuliaga kule kwa Makhirikhiri

Kweli wakati ukuta, tumetoka mbali sana
 
Mzee ruksa hiyo.

Ni moja ya move za mwisho mwisho za mzee ruksa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995

TRA imeanzishwa mwezi wa nane mwaka 1995, Mkapa alichaguliwa kuingia madarakani mwezi wa kumi na moja mwaka huo
Nilisikia hivyo maana kipindi hicho nakaribia la kwanza, ni muda mrefu sana mpaka sasa nimekuwa babu.
 
Siyo wewe tu, wengi wanaaminishwa kuwa TRA aliianzisha BWM lakini ukweli ni kuwa aliianzisha AHM. Unaweza kucheki hata kwenye website ya TRA kuhusu lini ilianzishwa.
Kombora la taifa nakubaliana na wewe, tatizo tunadanganywa na sisi siyo watafiti tuna kubali, binafsi nifundishwa chuo kwenye tax kuwa TRA ilianzishwa awamu ya 3, 100% nilikuwa naamini hivyo. Asante sn mkuu
 
Siyo wewe tu , wengi wanaaminishwa kuwa TRA aliianzisha BWM lakini ukweli ni kuwa aliianzisha AHM
Unaweza kucheki hata kwenye website ya TRA kuhusu lini ilianzishwa
Mkapa alifanya reforms ndani ya TRA na siyo kuianzisha...kuna watu waliliwa vichwa pale haijawahi kutokea...walipelekewa wachunguzi pale kilichotokea kilikuwa ni kilio Cha kufa mtu..
 
Kupeana zawadi dhahabu,mikopo chuo/bodi ya mikopo,Tanesco ilivyouzwa kwa wa South. Mkapa Baba wa ubinafisishaji usio na Tija kwa taifa.
Kuuzwa nyumba za serikali,sasa kutwa wanahangaika kujenga nyumba mpya.
 
Kabla ya TAKURU(PCB) ile ya Jenerali Kamazima mapambano ya Rushwa yalikua yanaongozwa na Kikosi Cha Kupambana na Rushwa(Task Force) iliyokua inahusisha Polisi na UWT

Ndio maana mpaka leo TAKUKURU hawana chuo bado mafunzo yao mengi wanachukuliaga kule kwa Makhirikhiri

Kweli wakati ukuta, tumetoka mbali sana
Sidhani,nakumbuka mwaka 1993,nikiwa obay line polisi,,nikiwasikia maafande wakipiga story jinsi afande mmoja aliwekewa mtego wa kukamatwa rushwa,,akawaweka maofisa wa PCB on gunpoint,kabla hajadandia taxi na kukimbia,
 
Kubwa ni Sukari aisee

Sukari haikupanda Bei Wala kuadimika...Kilo ya Sukari ilikuwa shs 600 kwa miaka 10.

Magufuli hapa anafeli wapi?
 
Sidhani,nakumbuka mwaka 1993,nikiwa obay line polisi,,nikiwasikia maafande wakipiga story jinsi afande mmoja aliwekewa mtego wa kukamatwa rushwa,,akawaweka maofisa wa PCB on gunpoint,kabla hajadandia taxi na kukimbia,

Hawakua PCB kama PCB haikuwepo ilikua inaitwa Kikosi Cha Kupambana na Rushwa

And yes kuna changamoto kubwa sana kukamata Rushwa inayotendeka na vyombo vingine vile
 
Nadhani enzi hizo JK alikua waziri.wa fedha
mzee ruksa hiyo.

Ni moja ya move za mwisho mwisho za mzee ruksa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1995

TRA imeanzishwa mwezi wa nane mwaka 1995, Mkapa alichaguliwa kuingia madarakani mwezi wa kumi na moja mwaka huo
 
Alifuta kodi ya kichwa, ada ya shule ya msingi na umitashumta, alifuta kodi ya vipande vya baiskeli. Aloanzisha kodi ya VAT.

Alirasimisha uwepo wa TISS na kujaribu kuiondoa kwenye makucha ya mlengo wa kisiasa (japo inaonekana imerudi kulekule)

Kwa kifupi aliamini zaidi kwenye taifa lenye taasisi imara, biashara inafanywa na sekta binafsi huku serikali ikiwa msimamizi. Tukumbuke kuwa taasisi ni endelevu lakini viongozi wanapita.
 
Rais Mkapa ndiye alianzisha "Hotuba kwa Taifa' kila mwisho wa mwezi kutokea IKULU.Akielezea Taifa kazi na shughuli zilizofanywa na Serikali ķila mwisho wa mwezi.

Naombea Ikulu ya Chamwino iwe na chumba cha habari, tuwe tunapata Hotuba kwaTaifa mubashara,maana siku hizi ndio muhimu kuliko wakati wowote ule,ili kuwafikia Watanzania wote kwa haraka zaidi.
 
Back
Top Bottom