Baadhi ya Mama wa kambo hawana jema

Baadhi ya Mama wa kambo hawana jema

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,615
Reaction score
2,264
Wakuu, leo ningependa tujadili juu ya huyu mlezi asie na bahati mbele ya jamii. (mama wa kambo)imekua ni nadra sana kwa jamii ama mtu mmojammoja kuonesha heshima au kuwa na shukrani kwa huduma ya malezi inayotolewa na mama wa kambo. siku zote yeye amekua niwakukosolewa na kulaumiwa tu,

Hebu tuchukulie pale mama wa kambo anapokua karibu na mtoto huyu wa mumewe, watu tunaona anamnyanyasa na pale anapomuacha huru watu tunaona hamjali matokeo yake mlezi huyu anapoteza msimamo na kushindwa kumlea mtoto vizuri na matokeo yake mtoto anakosa malezi bora.

Yote hayo yanatokea si kwasababu hawana mapenzi ya kweli kwa watoto wa waume zao bali ni kwasababu ya kutaka kuiridhisha jamii inayowazunguka ambayo inawatu wenye mitazamo tofauti. hivi ni kwanini mama wa kambo hathaminiwi na hapewi heshima inayostahili?
 
Toka tumeishi duniani na kuwepo kwa wamama hawa mnaowaita wakambo, jamii imekua ikiwaona wakarofi wasiofaa kutokana na wao wenyewe walivyoishi na wahusika waliowasababisha wawe hivyo.
 
Toka tumeishi duniani na kuwepo kwa wamama hawa mnaowaita wakambo, jamii imekua ikiwaona wakarofi wasiofaa kutokana na wao wenyewe walivyoishi na wahusika waliowasababisha wawe hivyo.
chuki dhidi yao imepitiliza, kiasi kwamba akina mama sasa wamekua waoga kubeba hilo jukumu.
 
Asilimia kubwa watoto wenu wanateswa na mnayataka wenyewe...kuzalisha mabinti za watu afu hamtaki kuwaweka ndani
 
chuki dhidi yao imepitiliza, kiasi kwamba akina mama sasa wamekua waoga kubeba hilo jukumu.
"...ni kutokana na wao wenyewe walivyoishi na wahusika waliowasababisha wawe hivyo"
 
Mimi binafsi naona hakuna kazi nzito kama kuwa mama wa kambo, sina shida na mtu aliyezaa kabla ya ndoa ila penye umama wa kambo pagumu sana. Mkuu umesema kweli kabisa
 
Asilimia kubwa watoto wenu wanateswa na mnayataka wenyewe...kuzalisha mabinti za watu afu hamtaki kuwaweka ndani
Wapo wanaoolewa kwa upendo wa hali ya juu lakini baada ya muda hulazimisha kuachwa na kuacha watoto kwa mume.
 
Back
Top Bottom