Baadhi ya malipo Serikalini/Halmashauri hayana mantiki

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Kuna malipo ambayo sio kodi, matharani ni tozo, ushuru au ada na hakuna huduma ambayo mtu anaipata kutokana na malipo hayo zaidi ni kumuongezea mwananchi mzigo kwa kumuongezea gharama za maisha. Angalia mfano ufuatao

Katika stendi za mabasi, mathalani Stendi ya Magufuli, unatakiwa kulipa Tsh. 300 na hakuna huduma unaipata kujustfy malipo hayo, mtu mwenye tiketi anapita bila kulipa. Inawezekana unaenda ndani kukata tiketi, na unalazimika kulipa fedha hiyo ambayo imeshakuwa mazoea kwenye stendi nyingi nchini

NI hela ndogo, lakini kuna watu hata nauli wanasaidiwa ili kuweza kusafiri, ni vyema ofisi za mabasi ziwe nje, ili mtu akate tiketi aingie bure ili kupata huduma kama ni ya usafiri au nyinginezo

Gharama nyngine kwenye Stendi

Mbali na kulipa Tsh. 300 kwenye stendi bado mtu huyu atalipa Tsh. 300 kwenda haja. Je Tsh. 300 ya mwanzo ililipwa kwa ajili ya nini, kama ni malipo ya huduma za ndani kwa nini mtu asilipe Tsh. 300 ambayo itamuhakikishi kupata huduma zote za ndani ya stendi ikiwemo kwenda haja?

Fikiria hili!

Mama mwenye mtaji wa Tsh. 30,000 anauza matunda ndani ya stendi ambapo anakaa kuanzia saa 11 asubuhi hadi saa mbili usiku, anaweza kwenda haja mara ngapi, anapata faida gani kwenye biashara ndogo kama hii.

Masikini analia zaidi

Signed OEDIPUS
 
Wabongo mnapenda kujilizaliza kama mbwa koko.

Hata wakifanya kuingia humo ndani ni bure ukujanhapa kulia lia na kulalamika.

Humo stand patajaa v8baka itakuwa ni kuibiana mwanzo mwisho na vjrugu zisizokuwa na maana yoyote tena kwa watu ambao hawananhata chankufanya humo stand.

Ukitaka kutolipa hiyo 300 kata ticket nje, ofisi za mabus zomejaa mpaka Mbagala na Mwananyamala.
 
Back
Top Bottom