Baada ya ziara ya Rais Kenyatta, Tanzania iko tayari kufungua mipaka yake ili majirani zetu ktk EAC waje kulima na kuchunga?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..waTz tumekuwa na msimamo wa muda mrefu kwamba ardhi ya Tz itabakia kuwa ya waTz.

..msimamo huo umewafanya ndugu zetu ktk jumuiya ya afrika mashariki kutuchukulia kama wakwamishaji wa muungano na ustawi wa jumuiya yetu.

..nimefuatilia ziara ya Raisi Kenyatta Tanzania, na nimesikiliza hotuba yake na ile ya Raisi Magufuli.

..Picha niliyoipata ni kuwa huenda " tumeshawishiwa " kuachana na msimamo wetu wa awali kuhusu kulinda ARDHI yetu, na AJIRA za watu wetu.

..Huenda tunakwenda kufungua mipaka yetu ktk masuala ya ardhi, utalii, na soko la ajira.

..Je, muelekeo huo mpya una manufaa kwa waTz ,au utaleta maumivu kwetu?

Cc Malcom Lumumba,Nguruvi3, Pascal Mayalla, Magonjwa Mtambuka, Ngongo, Pohamba
 
Mkuu hayo mengi yaliyoongelewa yapo kwenye mikataba na bado hayatekelezwi. Kwa ujumla walikuwa wanafurahisha genge na hakuna lolote litatekelezwa. Ukishaona jambo lipo kwenye mkataba na bado halitekelezwi, litatekelezwa vipi kwenye mazungumzo ya ziara binafsi za viongozi? Jamaa alimuita Kenyatta amringishie uwanja wa ndege, but nothing serious.
 
..Picha niliyoipata ni kuwa huenda " tumeshawishiwa " kuachana na msimamo wetu wa awali kuhusu kulinda ARDHI yetu, na AJIRA za watu wetu.

..Huenda tunakwenda kufungua mipaka yetu ktk masuala ya ardhi, utalii, na soko la ajira....
Unaposema "huenda" una maana gani?
 
..waTz tumekuwa na msimamo wa muda mrefu kwamba ardhi ya Tz itabakia kuwa ya waTz.

..msimamo huo umewafanya ndugu zetu ktk jumuiya ya afrika mashariki kutuchukulia kama wakwamishaji wa muungano na ustawi wa jumuiya yetu.

..nimefuatilia ziara ya Raisi Kenyatta Tanzania, na nimesikiliza hotuba yake na ile ya Raisi Magufuli.

..Picha niliyoipata ni kuwa huenda " tumeshawishiwa " kuachana na msimamo wetu wa awali kuhusu kulinda ARDHI yetu, na AJIRA za watu wetu.

..Huenda tunakwenda kufungua mipaka yetu ktk masuala ya ardhi, utalii, na soko la ajira.

..Je, muelekeo huo mpya una manufaa kwa waTz ,au utaleta maumivu kwetu?

Cc Malcom Lumumba,Nguruvi3, Pascal Mayalla, Magonjwa Mtambuka, Ngongo, Pohamba

Kusema kweli kuna mambo huwezi kusema utaruhusu yoyote achukue sababu ya kuwa kwenye jumuiya ya EA. Pengine sheria ziwekwe kwa namna ambayo wawekezaji watalindwa, ili sio kila wazururaji.
Kwa jinsi Kenyatta alivyoongea, unaona kabisa anatamani biashara kwenye jumuiya yetu iongezeke. Suala la muhimu itaongezeka kwa taratibu gani?
Kuchukua ardhi yetu sio kusudio jema la kukuza muingiliano wa watu na biashara kwa mtazamo wangu. Kuna siku mbele ya safari linaweza kulera shida kubwa.
 
..baada ya kumlaani yule mbunge wa kenya.

..na mapokezi tuliyompa Raisi Kenyatta.

..je, tutaweza kushikilia msimamo wetu wa awali kuhusu ARDHI na AJIRA ktk EAC?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mambo ya kuongelea nyumbani kwako kama unaongea chumbani na mke wako kwa kisingizio cha kuongea na rafiki yako wakati mambo yenyewe yanahusu Taifa,huku ukijua kuwa utakacho kisema ni tamko la nchi na ni lazima litekelezwe na nchi, siku moja yatakuja kuigharim nchi.
 
Kusema kweli kuna mambo huwezi kusema utaruhusu yoyote achukue sababu ya kuwa kwenye jumuiya ya EA. Pengine sheria ziwekwe kwa namna ambayo wawekezaji watalindwa, ili sio kila wazururaji.
Kwa jinsi Kenyatta alivyoongea, unaona kabisa anatamani biashara kwenye jumuiya yetu iongezeke. Suala la muhimu itaongezeka kwa taratibu gani?
Kuchukua ardhi yetu sio kusudio jema la kukuza muingiliano wa watu na biashara kwa mtazamo wangu. Kuna siku mbele ya safari linaweza kulera shida kubwa.

..waTz tulilalamika yule mbunge alipodai wamachinga waTz walioko Kny watimuliwe.

..sasa waKny wakiruhusu wamachinga toka Tz, sisi tutatoa wapi moral authority ya kuzuia wafugaji wa Kny wasiingize mifugo yao Tz, au magari ya Kny yasiingize watalii ktk mbuga zetu?

..na kauli za Raisi Kenyatta ziliashiria kwamba ile misimamo ya awali inakwenda kuondoka. Sikumsikia JPM akiongea lugha tofauti.
 
..baada ya kumlaani yule mbunge wa kenya.

..na mapokezi tuliyompa Raisi Kenyatta.

..je, tutaweza kushikilia msimamo wetu wa awali kuhusu ARDHI na AJIRA ktk EAC?

Mkuu kuhusu Mapokezi nnadhani hili ni Suala la kidiplomasia zaidi ,hatujui walicho zungumza wao Binafsi(Nje ya Taarifa zilizopo) hivyo inawezekana kuna alie Omba Radhi japo hatuna hakika kama ndio njia sahihi ya kuyamaliza Matatizo baina yetu kama Majirani..

Suala la Msimamo bado ni Kitendawili ,una kumbuka ziliwahi kuletwa Taarifa huku kuhusu Askari wa Rwanda walio waua Wananchi wetu na (Binafsi) sikusikia Taarifa ya Serikali kwenye hili kama kuna mwenye nayo tuna omba atuwekee
 
..waTz tulilalamika yule mbunge alipodai wamachinga waTz walioko Kny watimuliwe.

..sasa waKny wakiruhusu wamachinga toka Tz, sisi tutatoa wapi moral authority ya kuzuia wafugaji wa Kny wasiingize mifugo yao Tz, au magari ya Kny yasiingize watalii ktk mbuga zetu?

..na kauli za Raisi Kenyatta ziliashiria kwamba ile misimamo ya awali inakwenda kuondoka. Sikumsikia JPM akiongea lugha tofauti.

Kuna mambo magumu sana kuyaelezea papo kwa papo. Maana yanahitaji maandalizi ya kina. Nina shaka kama tunaweza kufikia huko kwa haraka kiasi hicho.
 
..Tz utamaduni wetu ni kuwa kukiwa na conflict baina ya kauli ya Raisi na sheria zetu, kinachotekelezwa ni kauli ya Raisi.
 
..waTz tumekuwa na msimamo wa muda mrefu kwamba ardhi ya Tz itabakia kuwa ya waTz.

..msimamo huo umewafanya ndugu zetu ktk jumuiya ya afrika mashariki kutuchukulia kama wakwamishaji wa muungano na ustawi wa jumuiya yetu.

..nimefuatilia ziara ya Raisi Kenyatta Tanzania, na nimesikiliza hotuba yake na ile ya Raisi Magufuli.

..Picha niliyoipata ni kuwa huenda " tumeshawishiwa " kuachana na msimamo wetu wa awali kuhusu kulinda ARDHI yetu, na AJIRA za watu wetu.

..Huenda tunakwenda kufungua mipaka yetu ktk masuala ya ardhi, utalii, na soko la ajira.

..Je, muelekeo huo mpya una manufaa kwa waTz ,au utaleta maumivu kwetu?

Cc Malcom Lumumba,Nguruvi3, Pascal Mayalla, Magonjwa Mtambuka, Ngongo, Pohamba

Tatizo letu Adhi yetu imekuwa kama mapambo tu sehemu ambazo hazilimwi na ni vichaka tu ni kwanini tusitafute watu walime na tuwe na mazao yakutosha viwandani badala ya kusema tu ni ya Watanzania pekee wakati 75% iko wazi. Tunachotakiwa ni kuwa na sheria nzuri badala ya sheria za miaka ya 60-70. Hatuwezi kuendeleza viwanda bila kuwa na kilimo cha uhakika. Watanzania wote tunakodishiwa lakini ni simple tu wangesema kwa wale ambao si Watanzania ni miaka 10 kukodi hivyo miji ikikuwa haikodishwi lakini tu kusiwe na usanii wa kutaka kutengenezewa mashamba. Hatuwezi kuendelea kioga kioga tu acha watu walime Ardhi haiendi mahali hata kama ni 40% tu tutakuwa walishaji wakuu SADC nzima
 
Kuongezee utaratibu wa sasa wa viwanda kupewa mashamba bure si mzuri ni bora tuite wakulima ambao watalipa kodi na kuongeza ushindani. Sababu mojawapo ya serikali kutoa mashamba bure kwa wenye viwanda ni kwasababu ni vigumu kupata malighafi ya uhakika ya kotosha
 
Back
Top Bottom