mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,301
- 733
Hoja nyingi za uzi huu zimejikita kuihukumu Yanga kwa kuzingatia matokeo ya zamani dhidi ya Ahly na timu za 'Arabuni' kwa jumla. Hayo ni makosa mawili makubwa. Kama isivyo sahihi kumsifu Rage kwa mazuri ya Bamchawi ndani ya Yanga, hawezi kulaumiwa Manji kwa kasoro za Madega. Ingekuwa hivyo, basi Dida na Yanga walifanya vyema jana kuliko Juma Muhina na wenzake kule Cairo 1982. Kila mtu atwishwe mzigo wake. Aidha, kufungwa ni kufungwa tu, iwe na 'Waarabu' au Wazungu. Iweje kioja Yanga kufungwa kwa mazingira magumu kama ya jana, lakini liwe ni jambo la kawaida Azam kutolewa kirahisi na Ferroviaro? Au kwa sababu si 'Waarabu' ni 'Wamakonde'? Haya yote yanaonyesha jinsi tunavyozama kwenye lindi la ubaguzi bila ya kujijua. Ubaguzi wa nani tumlaumu, lakini zaidi ni ubaguzi wa rangi.
La sivyo ni rahisi kubaini kwamba la jana lilikuwa ni pambano la timu mbili nzuri ambapo mmoja alipaswa kutolewa. Mpira huamuliwa kwa fiimbi, sio kwa mizani. Si lazima timu bora ndiyo ishinde. Na inaposhindwa, haisathili lawama.