MENGELENI KWETU
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 9,549
- 24,159
Safi sana Lema.
Wa Tz nani katuloga kama serekari imekubali kusaidia matibabu Ls litakuwa jambo jema tulipokee tunachohitaji sisi ni kuona Ls analejea katika hari yake na si vinginevyo tusitengeneze kauli zitakazo wafanya serekari kughaili jambo hili kwa kauli zetu
Wamekubali kwa sharti la mke wake kuomba kwanza msaada yaani maana yake asipoomba hawatoi ni kama msaada wenye mashartiSwali halijapata majibu, Mwanzo walikataa kumtibia kwa kuwa utaratibu haukufuatwa, Sasa hivi wapo tayari kumtibia!! Je ndo kusema utaratibu umefuatwa ?
Hauwezi ukawa na uchungu kumzidi mkewe. Yupo na anaona kinacho endelea. Hao ndugu wengine ukiwaona utawafahamu?Katika suala hili la Lissu...wapi familia yake? Yaani mama, baba mdogo au mkubwa, shangazi na mama wadogo? Wakina Lema ndo wamegeuka baba wadogo zake na wasemaji wa familia.
Ni vema familia ya Lissu ikamuondoa Lissu katika minyororo ya wanasiasa hadi hapo atakapopona. Awepo msemaji wa familia juu ya mwenendo wa afya ya mpendwa wao na wasiwaachie hawa mashakubimbi ndio wakawa wasemaji....ugonjwa wa Lissu umegeuka kuwa ngazi ya kujipatia umaarufu.
Taarifa ya Ummy Mwalimu ya kuitaka Famili ya Lissu kuandika barua kama wanaitaji matibabu ya Lissu. na kwamba Serikali ipo tayari kujibu Lissu sehemu popote Duniani. Kwanza aache Uongo na upotoshaji, Serikali haipo tayari, ndo maana Spika kwa kinywa chake alikataa kwamba wao hawapo tayari kumtibu Lissu katika Hospital ya naiorbi. Vilevile sio utaratibu pale Mbunge anapokuwa mgonjwa kwamba Familia ndo iandike barua. Katibu wa Bunge na Spika ndo wanapaswa.
Leo siku ya 14 Spika wa bunge wala katibu wa bunge hawajawahi kutembelea Familia wala kumtembelea Mgonjwa Hospitalini.
Spika aliugua sana hivi karibuni, Wakina Mwakyembe Mwandosya, na wengine wengi wa CCM, je Utaratibu ulikuwa wa kuandika barua? Leo siku ya 14 Serikali haijatoa chochote.
Ummy, Mwamie aliyekutuma kwamba tutamlinda kwa sala zetu, hatujashindwa kama Wanachama, Hatujashindwa kama Watanzania kuchanga Shilingi moja moja kumtibia Lissu. Sala inasaidia Uponyaji, lakini wanaofanya sala manwakamata.
Kumbuka Familia ya Lissu ni Watanzania wote wanaopenda Utawala wa sheria na Kidemokrasia. Famililia ya Lissu ni Watanzaina wote wanaoguswa na Mbunge kupigwa Risasi hadharani na bunge lisichukue hatua sitahiki. Hatujashindwa kumlipia matibabu, Tutachanga Shilingi MOja moja tutauza hata mali zetu ili Lissu asikose matibabu.
Nikwambie Ummy mwambie aliyekutuma na wewe usikubali kutumwa vitu kama hivi, unafahamu nini kinaendelea. Ndo sababu Serikali yenyewe pamoja na viongozi wa Bunge wamekosa usajili wa kuja kumsalimia Mbunge ambaye yupo taabani sababu wanajua jambo hili limetendwa na nani.
Vinginevyo Bunge lingekuwa la kwanza kumlilia Lissu sababu Lissu ni Familia ya Bunge na baadala yake leo ni siku ya 14 Spika wala Naibu Spika aliyekuja Hospitali. Hata Ulipoombwa Muongozo wa kuteua wabunge bungeni waje kumtembelea Lissu, naibu Spika alisema walioko huko Nairobi wanatosha.
Mbunge wa CCM aliyekuja kumjulia hali Lissu ni Lazaro Nyalandu, hakuna Mbunge wala kiongozi wa Serikali wala Wa CCM aliyekuja kumtembelea Lissu Hospitali.
Hivyo Mheshimiwa Ummy hizo ngonjera hazisaidii.