Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,236
Kwa niaba ya Wananchi wa Kyela nachukua nafasi hii kukushukuru Mh Rais kwa kutembelea Wilaya Yetu , ninaamini umeinjoi hali ya hewa nzuri ya eneo hilo , na bila shaka baada ya kuhitimisha safari yako utakuwa umebeba Mbasa na Mbelele kidogo kwa ajili ya kitoweo .
Kyela kama yalivyo maeneo mengine ya nchi inazo changamoto zake , ambazo viongozi waliopita wameshindwa kuzitatua
Namba 1 ni maambukizi ya Ukimwi , Kyela ni miongoni mwa Wilaya za Tanzania zinazoongoza kwa Maambukizi ya Ukimwi , Juhudi kubwa zinatakiwa ili kudhibiti Maambukizi kwa kuongeza nguvu kwenye elimu ya namna ya kudhibiti ugonjwa huu , sina hakika kama watu wako wamekueleza hili .
Jambo lingine ni njama zilizofanywa na watu wanaofahamika , za kuua Taasisi ya MANGO TREE , ambayo ilikuwa na jukumu la kusaidia watoto yatima kielimu kutokana na vifo vya ukimwi vya wazazi wao , Wauaji wa Taasisi hii bado wako hai na wengine umeendelea kuwateua , zifanyike juhudi za kurejesha Taasisi hii .
Halmashauri ya Kyela ilimiliki Soko kubwa sana katikati ya Mji , linalofahamika kama Soka la Wilaya , Lakini viongozi wa Halmashauri akiwemo Hunter Mwakifuna wakishirikiana na DED wa wakati huo walipora soko hilo na kulimilikisha kwa CHAMA CHA MAPINDUZI kinyume kabisa cha Sheria za nchi , sisi wana Kyela tunataka soko hilo lirudishwe mikononi mwa Halmashauri kama awali , na wote waliohusika kuipa ccm soko hili wakamatwe haraka (ukipenda nitakutajia majina yao , yumo Mwakyembe )
Mradi wa maji wa vijijini uliojulikana kama MAJI YA DANIDA urejeshwe na miundo mbinu irejeshwe ili kuwaepusha wananchi na Maji ya Madimbwi , aliyeua mradi huu atafutwe na akamatwe .
Suala la barabara kwa Kyela bado ni kitendawili , ukiacha ile iliyofadhiliwa na wazungu ya Nkuyu - Matema , bado barabara nyingi ni tete huku madaraja mengi yakiwa duni sana ! Kwa mfano , Daraja la mbao na mavyuma la Ipyana , mvua ikinyesha kidogo tu wananchi wanakaa roho juu , huwa halichelewi kupinda ama hata kuhama , tunaomba hili litatuliwe , Waletwe wakandarasi wenye uwezo watengeneze daraja la kudumu kwa kuzingatia mazingira halisi .
Itaendelea ......