Kipindi cha awamu ya tano katika kipindi cha miaka mitano nilipata kipara au uharaza, baada ya uchaguz 2020,niliwaza mwili utaanza kupata mvi.Mabadiliko haya ya kimwili yalitokana na kufanya kazi Sana lakini hela kidogo,wategemezi waliozoea kuwatoa laki moja, elfu 50,20,10 au 5 kipindi cha JK walilia na kusaga meno kwani hawakupata tena.Hakika kipindi cha awamu ya tano ckupata chochote cha maendeleo.
Likatokea la kutokea tukapata awamu ya Sita, miez ya mwanzo tulifarijika toka mwez wa nne mpaka wa Sita 2021 kidogo tulipata mapumziko, wategemezi wangu kijijini walianza kupata kidogo, hadi watz wakasema MAMA ANAUPIGA MWINGI. Mwez mgumu kupita yote ni mwez wa saba msamiati kila mtaa, kijiji, Mji ni neno TOZO, Wengi hawakulizoea Sasa lipo kila sehemu.
Ukiongelea tozo waulize wavuvi, waulize wauza mifugo, waulize mawakala wa mitandao ya simu, wauza mafuta n. k.Hakika wamejua kutupiga na wanatupiga hasa, ukienda kununua kitoweo cha nyama au samaki bei haikamatik, mzunguko wa hela haupo biashara zimedorora, hatuna tena tumaini.
Ukiachana na neno TOZO, tumeanza tena Kamatakamata ya viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.Tulipumzika kidogo, kwa Sasa tumerudi kulekule.Kazi iendelee kumbe lilikuwa na maana kubwa.Tafakari.