Ni mtu wa kukosea na kutumia muda mwingi kujitetea. Nakumbuka wakati mambo yanaenda kombo vigogo wastaafu walimjia juu lakini yeye alichukua muda mwingi kusema angeshangaa kama wangempongeza.
Wakati marais wenzake wa Afrika mashariki wameamua kuendelea na umoja wao bila yeye kushirikishwa, alienda bungeni kujitetea na kulalamika kwamba hapendwi na wenzake. Alitumia muda mwingi kujitetea badala ya kuonyesha amekosea wapi.
Sasa kuhusu hili la mchakato wa katiba mpya, juzi alitumia muda mrefu sana kujitetea baada ya kulivuruga bunge la katiba. Tujiulize rais wetu kama rais wetu aliwahi kukiri makosa. Ni binadamu gani asiyekosea? Miaka yote tisa hakuwahi kufanya kosa? kama aliwahi kukosea ni kwa nini hata mara moja hatujawahi kumsikia akikiri badala ya kujitetea na kuwasukumia wengine mizigo yake?
Tafakari!