Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,075
- 136,490
Binadamu bana!
Watu wakiwa kwenye lindi la mapenzi huwa wanaonana wazuri sana.
Unakuta labda mdada anamsifia sana jamaa alivyo mzuri.
Anakuwa na majigambo ya hapa na pale. Kwamba hataki wadada wenzie waone hata picha zake kisa anahofia kuibiwa kwa sababu jamaa ni 'mzuri', kwa mujibu wake.
Sasa penzi likishachuja na wahusika kumwagana, ghafla yule alokuwa mzuri eti anageuka kuwa mbaya.
Utasikia 'oh mtu mwenyewe kwanza mbaya', 'mtu mwenyewe wala sio mzuri', mtu mwenyewe ana kibamia, mtu mwenyewe ana matege, mtu mwenyewe hivi, mtu mwenyewe vile.
Hilo limenipelekea niwaze hivi ni maneno yepi ambayo ndo huwa ya kweli?
Ya wakati penzi limekolea au ya wakati penzi linapochuja?
Pia kauli kama hizo ni moja ya uthibitisho kuwa mapenzi bila uongo uongo nayo hayataenda vizuri.
Wakati mwingine labda huwa inambidi mtu amdanganye mwenzake walau kidogo tu ili mapenzi yao yaweze kwenda bila mushkili.
Wadau nyie mnalizungumziaje hilo suala?
Mshawahi kuwa 'wazuri' pindi penzi limekolea lakini mkaja kuwa 'wabaya' baada penzi kuchuja au kuisha?