Kansigo
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 2,670
- 2,156
Baada ya mama yake kuteuliwa, Ridhiwani anena
Thursday , 2nd Mar , 2017
Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete amefunguka baada ya mama yake jana kuteuliwa na Rais Magufili kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ridhiwan Kikwete amesema kuwa mama Salma Kikwete ni mwanamke wa shoka kwani amewezesha wasichana wengi nchini Tanzania kupata elimu na amekuwa mtetezi wa haki za wanawake hivyo anaamini kupata nafasi ya kuwa Mbunge itakwenda kuwezesha mapambano kuwa sheria rasmi.
"Umekuwa mtetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu. Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera sana kwa uteuzi. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena" aliandika Mhe. Ridhiwan Kikwete