Baada ya madaktari kusalitiana;Sasa inafuata zamu ya waandishi wa habari

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Sisi watanzania tutendelea kuteseka chini ya utawala huu wa ccm mpaka siku Yesu/Masia atakaporudi duniani.Taarifa iliyotolewa na madaktari wanaojiita waathirika wa mgomo ni usaliti mkubwa miongoni mwao na wanamanisha kuwa madai yao yote yalikuwa hayana msingi.Nafikia hatua ya kujiuliza hivi hawa wanatumika kisiasa au ni ugumu wa maisha baada ya kukaa mtaani bila kazi ndio sababu ya wao kuomba radhi.Hata hivyo, maneno walioyatumia katika kuomba radhi yanaashiria kuwa wanasukumwa na kitu cha zaidi na sio ugumu wa maisha tu baada ya kusimamishwa.Hivi kweli hawa wakati ule wa mgomo walikuwa hawajui walitendalo!Tuseme ile kauli ya kikwete kwamba hawana pa kukimbilia ndio inatimia?Hii inaleta picha gani kwa wafanyakazi wengine wa umma ambao nao wanalia maslahi duni?Sasa na nyinyi walimu mjipange,mwenzako akinyolewa wewe tia maji.

Baada ya madaktari kusalitiana, siku si nyingi, litaibuka kundi la waandishi wa habari kutangaza kujitenga na msimamo wa wenzao.Ule msimamo wao wa kususia habari za jeshi la polisi kwa siku arobaini uko mashakani kwani mbinu zipo nyingi za kuwafanya wasalitiane.Watanzania tuna udhaifu mkubwa sana katika kudai haki zetu.

Tusubiri kusikia nao wakimuomba radhi waziri Nchimbi kwa kitendo chao cha kumzomea hadharani.

Ni swala la muda tu kabla ya hawa nao kusalitiana.

Watanzani lazima tukubali ukweli kuwa, mabadiliko yoyote yana gharama zake na hivyo tujiandae kubeba gharama hizo.Bila kuwa tayari kubeba gharama hizo kamwe hatutafanikiwa.
 
wamenisikitisha sana.......... kwanza sura zao zinaonyesha walishakatatamaa hata kabla ya kugoma...........hivi ile jumuiya ikowapi.........wapi dr godbless na dr chitage.........
 
Hamuwezi kuwaelewa kwa sababu hamko katika position yao...

Mimi naamini hawa watu dhamira zao zimejaa fedheha na machungu ya maisha ila ndio hivyo serikali imeshika mpini na wao wameshika kwenye makali.

Dawa ya watumishi wote wa umma ni kuungana dhidi ya serikali ya chama hiki 2015.
 
Back
Top Bottom