Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wakili Tundu Lissu, ambayo ilipangwa kuendelea kusikilizwa tarehe 3 Novemba 2025, haikuweza kuendelea kama ilivyopangwa. Kesi hiyo iliahirishwa hadi 10
Novemba 2025, lakini hata tarehe hii ya leo Lissu hajafikishwa mahakamani.
Wakili wa Serikali, Thawabu Issa, ameieleza Mahakama kuwa wamewasiliana na Mkuu
wa Gereza la Ukonga na amewaambia kuwa Tundu Lissu hakufikishwa mahakamani kutokana na hali ya kiusalama. Aidha, Wakili wa Serikali ameeleza pia kuwa mashahidi waliopaswa kutoa ushahidi walikuwa wanatokea Ruvuma na Mbeya, lakini kutokana na hali ya usalama kutokuwa ya kuridhisha jijini Dar es Salaam, hawakuweza kusafiri kufika mahakamani.
Kutokana na hilo, upande wa Jamhuri uliomba ahirisho la siku 14 kwa mujibu wa kifungu
cha 302 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ukieleza kuwa kushindwa kwa
mashahidi kufika kulitokana na sababu za kiusalama.
Baada ya kusikiliza maombi hayo, Mahakama imekubali ombi la upande wa mashtaka
lakini imeahirisha kesi hadi tarehe 12 Novemba 2025 na sio siku 14 walizoomba kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji. Mahakama imeagiza upande wa Jamhuri kuhakikisha mashahidi wanakuwepo siku hiyo na Tundu Lissu afikishwe mahakamani.