Baada ya Kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, CHADEMA Kwenda Mahakamani

Hakuna kiongozi yeyote duniani aliyedhubutu kuwatawala wananchi wake kwa mabavu akafanikiwa... its a matter of time.
 
Hela za kuendeshea kesi watatoa wapi?? Maana mkwanja wote umekatwa kwa sababu walifukuzwa bungeni. Na hao wanaosign na kutoka dawa yao inakuja
Na ruzuku yote anachukua lowasa, ofisi za mikoani ziko hoi, ofisi za Kanda zimeufa, hata gari moja ya M4C haionekani
 
KUZUIWA kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahaki, anaandika Dany Tibason.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema kimepanga kuwafikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC) pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini (OCD).

Chama hicho kimetoa tamko hilo leo mkoani humo kutokana na kupigwa marufuku kuendesha mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya Bunge.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jella Mambo, Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na madai ya kuchoshwa na unyanyasaji unaofanywa na viongozi wa mkoa kuzuia mikitano yao ya siasa ya wapinzani.

Mambo amesema kuwa, chama hicho kimepigwa marufuku na uongozi wa Mkoa wa Dodoma kufanya mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya bunge.

Amesema, uongozi wa Chadema mkoa unakusudia kuwapeleka watu hao mahakamani ili mahakama iweze kutafusiri sheria na kasha kubaini kama kuna sheria yoyote ya masuala ya siasa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya bunge.

Mbali na hilo amesema, wanataka kujua kama kuna haki ya kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge na iweze kufafanua kama sheria inahusu Mkoa wa Dodoma tu au na mikoa mingine.

“Utamaduni wa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge ulianzishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi jambo ambalo alilenga kufifisha upinzani Dodoma baada ya kuona kasi ya upinzani inapamba moto,” amesema Mambo.

Wakati wa Dk. Nchimbi, aliiandikia barua Chadema iliyokataza kuendesha mikutano ya hadhara katika kipindi cha Bunge na kwamba, inapingana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

“Lengo hapa ni kukandamiza upinzani ambao unaonekana kupanda chati kila siku, hivyo wanatunyima kufanya mikutano yetu kwa visingizio vya Bunge.

“Lakini ukiangalia sheria ya vyama vya siasa inasema kuwa moja ya majukumu ya vyama vya siasa ni kufanya mikutano na mambo mengine kama hayo bila kujali kuna bunge au hakuna,” amesema Mambo.

Amesema kuwa, lengo la kwenda mahakani ni kutaka kupatiwa tafsili ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 ambayo itawasaidia kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikiletwa na watawala wa mkoa wa Dodoma ambao ni wateule wa chama cha mapinduzi.

“Huku ni kutaka kuipunguza nguvu chadema pamoja na upinzani kwa ujumla kwani wamekuwa wakitusumbua sana.

“Wengine tunapigwa na polisi lakini pia tunafunguliwa kesi zaidi ya tatu na tunashinda sasa hatutakiwi kuendelea na hali hii ndiyo maana tunataka kwenda mahakani ili kuweza kupatiwa tafsiri ya sheria hii,”amesema Mambo.

Amesema kuwa, kitendo cha Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru mashariki kutolewa bungeni kwa kuvutwa kama mwizi alipotoa hoja ya msingi ya kutaka kujadiwa kuondolewa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni unyanyasaji wa kijinsia na kumkosea adabu mtu ambaye ni mwakilishi wa wananchi.
Muwe mnajua mnachokiongea. Sasa Nasari katolewa na wanaume wenzake hapo kuna unyanyasaji gani wa kijinsia?
 
Chadema naona kama zama zao zinaisha kiaina hivi. Anyways, tusubiri labda kutakuwa na mabadiliko mbele.

Mbowe namshangaa sana,yeye anasubiri nini si aende huko mahakamani,sasa anabwabwaja nini??

Yaani huyu jamaa anapenda sana kuongelea juu ya mti.
 
Me nlidhan wamejifunza kutoka kwenye msiba wa Mawazo, kumbe bado? Magu nae yupo tu wala hata hakemei upuuzi huo... Kweli CCM kimezeeka vbaya... Haya yetu macho na masikio.
Machadema akili mbovu kabisa, yameshindwa kujiheshimu bungeni, hayajui yametumwa nini na wana majimbo wao, kutwa yanadandia hoja hewani na kuzifanya ajenda zao,! Mtaishi kwa matukio hadi lini?
 
KUZUIWA kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeahaki, anaandika Dany Tibason.

Kutokana na hatua hiyo, Chadema kimepanga kuwafikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC) pamoja na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini (OCD).

Chama hicho kimetoa tamko hilo leo mkoani humo kutokana na kupigwa marufuku kuendesha mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya Bunge.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jella Mambo, Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na madai ya kuchoshwa na unyanyasaji unaofanywa na viongozi wa mkoa kuzuia mikitano yao ya siasa ya wapinzani.

Mambo amesema kuwa, chama hicho kimepigwa marufuku na uongozi wa Mkoa wa Dodoma kufanya mikutano ya hadhara wakati wa vikao vya bunge.

Amesema, uongozi wa Chadema mkoa unakusudia kuwapeleka watu hao mahakamani ili mahakama iweze kutafusiri sheria na kasha kubaini kama kuna sheria yoyote ya masuala ya siasa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya bunge.

Mbali na hilo amesema, wanataka kujua kama kuna haki ya kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge na iweze kufafanua kama sheria inahusu Mkoa wa Dodoma tu au na mikoa mingine.

“Utamaduni wa kuzuia mikutano ya kisiasa wakati wa vikao vya Bunge ulianzishwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi jambo ambalo alilenga kufifisha upinzani Dodoma baada ya kuona kasi ya upinzani inapamba moto,” amesema Mambo.

Wakati wa Dk. Nchimbi, aliiandikia barua Chadema iliyokataza kuendesha mikutano ya hadhara katika kipindi cha Bunge na kwamba, inapingana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

“Lengo hapa ni kukandamiza upinzani ambao unaonekana kupanda chati kila siku, hivyo wanatunyima kufanya mikutano yetu kwa visingizio vya Bunge.

“Lakini ukiangalia sheria ya vyama vya siasa inasema kuwa moja ya majukumu ya vyama vya siasa ni kufanya mikutano na mambo mengine kama hayo bila kujali kuna bunge au hakuna,” amesema Mambo.

Amesema kuwa, lengo la kwenda mahakani ni kutaka kupatiwa tafsili ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 ambayo itawasaidia kuondokana na kero hiyo ambayo imekuwa ikiletwa na watawala wa mkoa wa Dodoma ambao ni wateule wa chama cha mapinduzi.

“Huku ni kutaka kuipunguza nguvu chadema pamoja na upinzani kwa ujumla kwani wamekuwa wakitusumbua sana.

“Wengine tunapigwa na polisi lakini pia tunafunguliwa kesi zaidi ya tatu na tunashinda sasa hatutakiwi kuendelea na hali hii ndiyo maana tunataka kwenda mahakani ili kuweza kupatiwa tafsiri ya sheria hii,”amesema Mambo.

Amesema kuwa, kitendo cha Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru mashariki kutolewa bungeni kwa kuvutwa kama mwizi alipotoa hoja ya msingi ya kutaka kujadiwa kuondolewa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ni unyanyasaji wa kijinsia na kumkosea adabu mtu ambaye ni mwakilishi wa wananchi.
Hawana jipya hao. Duh pole Sana CDM
 
Na ruzuku yote anachukua lowasa, ofisi za mikoani ziko hoi, ofisi za Kanda zimeufa, hata gari moja ya M4C haionekani
Mkuu umenikumbusha yale ma pick up ya M4C kweli siyaoni au yalikuwa ya mtu binafsi.
 
Hela za kuendeshea kesi watatoa wapi?? Maana mkwanja wote umekatwa kwa sababu walifukuzwa bungeni. Na hao wanaosign na kutoka dawa yao inakuja
Pole sana yaonekana haujui chochote kuhusu uendeshaji wa shughuli za vyama vya siasa.
 
Ni wazo zuri sana kuipeleka Ccm mahakamani ila, angalizo ni kwamba watazuia nchi nzima kwa kisingizio cha kuna kesi mahakamani.
 
Hii ni njia sahihi kabisa, hata wakati wa msiba wa Kamanda Mawazo walibana mahakama ikatusaidia
Si vizuri wananchi wakipoteza imani na Mahakama kama walivyopoteza kwa POLISI,hebu mahakama wasimamie haki,wajaribu kuiga hata kwa majirani zetu KENYA.
 
Back
Top Bottom