Baada ya Kuzuiwa kufanya mikutano ya kisiasa mkoani Dodoma, CHADEMA Kwenda Mahakamani

Hela za kuendeshea kesi watatoa wapi?? Maana mkwanja wote umekatwa kwa sababu walifukuzwa bungeni. Na hao wanaosign na kutoka dawa yao inakuja
Hivi huu mpango wa kusaini na kuondoka ili muradi walipwe posho si wizi huu?
 
Unakosea sana, wewe ni mzee mwenzangu unazeeka vibaya, au unataka mtifuano tuwafaidishe watoto wa jukwaani!!!
Oh,we ni bingwa wa mtifuano. Is that the problem? Kama tunabishana,lazima uanze kwa kujitambulisha. Kwa nini mimi nibishane na mtu ambaye amevaa mask? That is chaos. Ndio maana nilikuwa nauliza yule mtoto ni nani.
 
Viongozi wa kitaifa CHADEMA wamekubaliana kufungua kesi mahakamani kupinga zuio la mikutano ya hadhara lililotolewa na Jeshi la Polisi.

===========

pic+mbowe.jpg

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe.

Kahama. CHADEMA kimesema leo kinatarajia kufungua kesi Mahakama Kuu kanda ya Mwanza dhidi ya Polisi, kupinga zuio la maandamano mikutano ya hadhara ya kisiasa.

Akizungumza mjini Kahama jana, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema mikutano ya hadhara ni haki ya kikatiba na hawatanyamaza inapozuiwa na mtu, au mamlaka yoyote.

“Tutapambana kwa njia na nguvu zote kulinda demokrasia nchini, hata kama itabidi kufia uwanjani. Ikibidi kwenda mahakamani kudai haki hiyo tutafanya hivyo.” alisema

Hata hivyo, Mbowe hakuwa tayari kuthibitisha taarifa za CHADEMA kufungua kesi jijini Mwanza, leo.

Mawakili wa Chadema akiwamo Peter Kibatala na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu walitarajiwa kuwasili Mwanza jana tayari kutoa ushauri wa kisheria na kufungua kesi.

Chanzo: Mwananchi
 
Sawa kabisa maana demokrasia na katiba zinachezewa, na waliochaguliwa kutuongoza na wakaapa kwa katiba hiyohiyo wanaona haya kuitetea
 
KENYA WAMEFANIKIWA! lAKINI HAPA MAHAKAMA ZETU NA KUINGILIWA NA DOLA SIJUI!

Sheria ya Kenya na hapa kwetu ni tofauti. wangeomba kibali sehemu kama moshi wangepewa kule kanda ya ziwa bado kulikuwa na sababu. Ni sawa na kuomba kibali cha maandamano Zanzibar huwezi pata.
 
Maamuzi mazuri mahakama itaamua kama ni sahihi chama cha siasa kukaa bila kufanya mikutano.
 
Viongozi wa kitaifa Chadema wamekubaliana kufungua kesi mahakamani kupinga zuio la mikutano ya hadhara lililotolewa na Jeshi la Polisi. NIPASHE ONLINE
Hiyo ndiyo itakuwa ni dawa ya kudumu kwa hili jeshi letu la polisi.wafanye kama kina odinga kenya waliamua kuifikisha mahakamani polisi na mahakama ikawapiga pini polisi na kuwaruhusu wapinzani kufanya mikutano yao
 
Maamuzi mazuri mahakama itaamua kama ni sahihi chama cha siasa kukaa bila kufanya mikutano.
Wakikutana na jaji mwenye uchungu na nchi hii huo ndio utakuwa mwanzo wa polisi kujichukulia sheria mkononi ya kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani
 
Sheria ya Kenya na hapa kwetu ni tofauti. wangeomba kibali sehemu kama moshi wangepewa kule kanda ya ziwa bado kulikuwa na sababu. Ni sawa na kuomba kibali cha maandamano Zanzibar huwezi pata.
Kanda ya ziwa kuna tatizo gani wakati mlituaminisha kuwa wale waliofanya uhalifu ni majambazi tu?
 
Nyinyi nyumbu mmetuchosha kila siku kulalamika tu,.
Sasa fanyeni nyumbu migration muhamie nchi yoyote isiyo na kodi.
 
Back
Top Bottom