ProjectPombe
Member
- Aug 29, 2013
- 49
- 51
Mada imeletwa for opinion polls! Ili watu fulani wasafishwe na kuhalalishwa!!
Ama kweli 'Nji' hii inaendeshwa ki-zuzu sana!!!
PP
Ama kweli 'Nji' hii inaendeshwa ki-zuzu sana!!!
PP
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuipanga upya safu ya Baraza lake la Mawaziri wakati wowote, huku baadhi ya wabunge na mawaziri wakitakiwa kusitisha mapumziko yao ya mwisho wa mwaka na kurejea jijini Dar es Salaam haraka.
Miongoni mwa wabunge waliositisha mapumziko yao na kurejea nchini ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa nchini Afrika Kusini na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Uswisi.
Wabunge hao walipoteza nafasi zao za uwaziri baada ya ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuwagusa mawaziri hao kwamba walishindwa kuwajibika katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Dk. Nchimbi anapewa nafasi ya kurejea kwenye Baraza la Mawaziri kutokana na kushiriki kwake kuipinga operesheni hiyo, ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, na kwamba alishawahi kumuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiipinga.
Kwa upande wake Kagasheki, anatajwa kurudi kwenye Baraza la Mawaziri kutokana na kubainika kwamba hakuwa na kosa na kwamba operesheni hiyo ilitekelezwa zaidi kijeshi na haikuwa chini ya wizara yake moja kwa moja.
Aidha Kagasheki anatajwa kuwa mmoja wa waliokuwa mawaziri hodari kutokana na uwezo wake wa kufuatilia mambo, ambapo akiwa ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, alianza harakati za kukomesha biashara haramu ya pembe za ndovu.
SOURCE:mtandao-net.blogspot.com
UNAIONAJE HIYO?
Huyo mzee Kagashjeki haa mimi naomba sana tafadali naomba Mungu arudi. Kwanza pia kaonyesha nidhamu ya hli a juu hata baada ya tukio
Kagasheki "Yes", Nchimbi "No"..
Kama Nchimbi anarudi ina maana Pinda anapigwa chini. Kumrudisha Nchimbi ni kukubali kuwa kweli alimwandikia barua PM lakini PM akasema wapigwe tu tumechoka na hili ni kosa kubwa ambalo katika nchi zinazojua wajibu wa viongozi anatakiwa kufikishwa mahakamani na hivyo hafai kuwa Waziri Mkuu
nchimbi?? aliandika barua kwa waziri mkuu kuipinga hiyo hoja,alipewa jibu gani?? iwapo yeye ataonekana safi kwa njia hiyo basi yule aliyepewa barua anamakosa(waziri mkuu).pinda alichukua maamuzi gani baada yakupokea barua yq nchimbi? kama hakuifanyia kazi huo ni uzembe..acheni kuwasafisha kirahisi hivi
nchimbi?? aliandika barua kwa waziri mkuu kuipinga hiyo hoja,alipewa jibu gani?? iwapo yeye ataonekana safi kwa njia hiyo basi yule aliyepewa barua anamakosa(waziri mkuu).pinda alichukua maamuzi gani baada yakupokea barua yq nchimbi? kama hakuifanyia kazi huo ni uzembe..acheni kuwasafisha kirahisi hivi
Mimi binafsi niliupenda sana utendaji wa Kagasheki
Hivi mimi nikisema kuwa rais ndiyo alipaswa kujiwajibisha au kuwajibishwa je,nitakuwa na kosa? Embu chukulia naye pinda alimpelekea kikwete,na kikwete alipuuza unadhani si yeye ndiye tatizo? Pia kama yeye ndiye alibariki hiyo operesheni c ni kosa la pili hilo la kumfanya aachie kitengo? Wabunge wetu huko DDM they are nonsense,wanamuogopa kikwete badala yake wana waya waya tu.