Baada ya kuwajibishwa, dk. Nchimbi na Kagasheki kurudi tena barazani!!

scholarsway

Member
Jul 18, 2013
25
0
images.jpg
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuipanga upya safu ya Baraza lake la Mawaziri wakati wowote, huku baadhi ya wabunge na mawaziri wakitakiwa kusitisha mapumziko yao ya mwisho wa mwaka na kurejea jijini Dar es Salaam haraka.

Miongoni mwa wabunge waliositisha mapumziko yao na kurejea nchini ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa nchini Afrika Kusini na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Uswisi.
Wabunge hao walipoteza nafasi zao za uwaziri baada ya ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuwagusa mawaziri hao kwamba walishindwa kuwajibika katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.

Dk. Nchimbi anapewa nafasi ya kurejea kwenye Baraza la Mawaziri kutokana na kushiriki kwake kuipinga operesheni hiyo, ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, na kwamba alishawahi kumuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiipinga.

Kwa upande wake Kagasheki, anatajwa kurudi kwenye Baraza la Mawaziri
kutokana na kubainika kwamba hakuwa na kosa na kwamba operesheni hiyo ilitekelezwa zaidi kijeshi na haikuwa chini ya wizara yake moja kwa moja.

Aidha Kagasheki anatajwa kuwa mmoja wa waliokuwa mawaziri hodari kutokana na uwezo wake wa kufuatilia mambo, ambapo akiwa ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, alianza harakati za kukomesha biashara haramu ya pembe za ndovu.

SOURCE:mtandao-net.blogspot.com
UNAIONAJE HIYO?
 
duchi

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,766
0
tena ikiwezekana warudishwe kwenye wizara zilezile ila badalishane.
 
Acuity

JF-Expert Member
Aug 13, 2013
391
170
hahahaa... Tanzania bhana, kwamba hakuna watu wengine wenye sifa??? Nipeni mimi muone kama siwezi....
 
ichenjezya

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
1,007
2,000
Kwani katika nchi hii yenye watu mil 40+ hakuna watu wengine wa kuingia kwenye hilo baraza,zaidi ya hao waliotoka kuanza rotation,hii ni dharau kwa watanzania for real....
 
Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,404
2,000
Kama Nchimbi anarudi ina maana Pinda anapigwa chini. Kumrudisha Nchimbi ni kukubali kuwa kweli alimwandikia barua PM lakini PM akasema wapigwe tu tumechoka na hili ni kosa kubwa ambalo katika nchi zinazojua wajibu wa viongozi anatakiwa kufikishwa mahakamani na hivyo hafai kuwa Waziri Mkuu
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Tunacheza Mduara! katika population ya watu milioni 45 tung'ang'ane na watu haohao kila kukicha na hata pale tunapopata uhakika kuwa wana udhaifu unaopita kiasi!
 
MWANAKA

JF-Expert Member
Oct 4, 2013
4,288
2,000
bora warudi aise kiukweli nilisikitika sana kusikia kagasheki akisema kwa huzuni kwamba ameamua kustep down
Lakini pia nina wasiwasi sana na utendaji wao wa kazi endapo watarejeshwa kwenye wizara hizo hizo
Mashaka haya yanakuja kwa kuiona ile dhana ya utendaji kazi kwa woga kutokana na haya yaliyowakuta
Kwa hiyo ningemshauri raisi wangu awape wizara zingine na si zile walizokuwa wanatumikia
Kwa upande wa ima pia na mwamwamini kwa utendaji kazi wake ingawa si siri kwamba kwa nafasi yake alijitengenezea maadui wengi sana
Bila shaka mtakumbuka ile picha ya kutengeneza aliyowekwa hapa akiwa na mmoja ya watu wanaosadikika kuwa ni vnara wa madawa ya kulevya
Kwa maana hiyo basi ushauri wangu kwa raisi ni kwamba Ima apangiwe wizara nyingine ili walau apumue kwa zigo zito alilokuwa amelibeba kwa muda mrefu ambalo kwa kiasi kikubwa limempa maadui wengi sana
Ima ni mchapa kazi makini na mahili na kwa kweli si mtu wa kukurupuka na kwa sifa hii ndio maana jk aliamua kumpa wizara nyeti hii ya mambo ya ndani
NI HAYO TU
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,162
2,000
...ya nini kuendelea kula matapishi...!
mbona kuna watendaji wengi na wazuri ndani ya chama chao... mapinduzi...!
 
MWANAKA

JF-Expert Member
Oct 4, 2013
4,288
2,000
naunga mkono kagasheki
kurudi ila nchimbi hapana apumzike.

Nafiri sasa naeleweka kwa mliosoma mapendekezo yangu hapo juu
Kwa wizara hii ya mabo ya ndani ni kama vile ndo umepewa kuwa mwalimu wa nidhamu shuleni hakuna hata siku moja wanafunzi watakupenda na hii ndio waizara aliyokuwa nayo Ima huwezi kutegemea watu wakamtamka vizuri hata kama angekuwa nani
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,626
2,000
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuipanga upya safu ya Baraza lake la Mawaziri wakati wowote, huku baadhi ya wabunge na mawaziri wakitakiwa kusitisha mapumziko yao ya mwisho wa mwaka na kurejea jijini Dar es Salaam haraka.

Miongoni mwa wabunge waliositisha mapumziko yao na kurejea nchini ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa nchini Afrika Kusini na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Uswisi.
Wabunge hao walipoteza nafasi zao za uwaziri baada ya ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuwagusa mawaziri hao kwamba walishindwa kuwajibika katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.

Dk. Nchimbi anapewa nafasi ya kurejea kwenye Baraza la Mawaziri kutokana na kushiriki kwake kuipinga operesheni hiyo, ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, na kwamba alishawahi kumuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiipinga.

Kwa upande wake Kagasheki, anatajwa kurudi kwenye Baraza la Mawaziri
kutokana na kubainika kwamba hakuwa na kosa na kwamba operesheni hiyo ilitekelezwa zaidi kijeshi na haikuwa chini ya wizara yake moja kwa moja.

Aidha Kagasheki anatajwa kuwa mmoja wa waliokuwa mawaziri hodari kutokana na uwezo wake wa kufuatilia mambo, ambapo akiwa ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, alianza harakati za kukomesha biashara haramu ya pembe za ndovu.

SOURCE:mtandao-net.blogspot.com
UNAIONAJE HIYO?

Huyo mzee Kagashjeki haa mimi naomba sana tafadali naomba Mungu arudi. Kwanza pia kaonyesha nidhamu ya hli a juu hata baada ya tukio
 
Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,650
2,000
Pinda na Nchimbi are mutually exclusive; haiwezekani ukamrudisha Nchimbi kwenye baraza la mawaziri hata kwa kigezo cha ushwahiba at the same time ukabaki na Pinda kama waziri mkuu!!! Mmoja wao lazima awajibike kwa kutofanya kazi yake inavyostahili; kumrudisha Nchimbi kwenye baraza la mawaziri ni kudhihilisha usemi wa Kapuya kuwa watoto wao wanauza madawa ya kulevya na hawakamatwi kwani ni serikali yao na mlinzi wao akiwa Nchimbi otherwise wangekamatwa alipokuwa waziri wa mambo ya ndani!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom