Baada ya kuumia, ulifanyaje?

Baada ya kuumia, ulifanyaje?

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,563
Nawasalimu wanajamvi,

Yamkini mlipendana sana,tena sana na mkapanga kuoana na kuwa na familia bora yenye watoto kadhaa.

Ikatokea mpenzi wako aidha akatangulia mbele ya haki au akakusaliti na kukuacha kabisa baada ya kukutana na jamaa anaejua matumizi ya mshedede na papuchi zaidi yako (kama wewe ni me) au amekutana na mwanamke anaejali,mnyenyekevu na mwenye kukata miuno kama pangaboi(kama wewe ni ke).

Kwa vyovyote vile uliumia (pole sana),sasa ulifanyaje baada ya hapo?

Na wewe uliekatisha ndoto za watu za kuoana unajisikiaje kumpoka mtu mpenziwe?

Kila leo watu wanaendelea kuumizwa,sasa basi mchango wako huenda ukawa ni somo kwa atakaeumizwa kwani badala ya kukimbila kujiua ama kujidhuru huenda hatua ulizochukua zikaokoa maisha yake kwa kufuata ama kufanya kama ulivyofanya wewe ulieumizwa na ukabaki salama.
 
MAISHA NI HISTORIA INAYOPASWA KUPITIWA KATIKA MATUKIO YA KILA NAMNA....
KUNA MAISHA BAADA YA KILA JAPO.CHA MUHIMU NI KUSAHAU AU KUPUUZIA NA KUSONGA MBELE.
 
Kuna kanuni inaitwa move on

Hii husaidi yaani unajipanga kuendelea na maisha mengine na kiukweli hii imesaidia wengi kuliko kuendelea na mpambano eti kugain your love back huku ukiendelea kuumia

Usipate depression za bure .ww move on utafanikiwa
 
Things happen for reason.
Ingawa inauma lakini hupaswi kujilaum zaidi kusonga mbele.life goes on.
Haya ni mambo common ambayo nadhani %kubwa wanayapitia.hivyo cha kujiambia kwamba hauko mwenyewe na kama wao waliweza ku give up na maisha yakaendelea why me!unakuta mtu analia na kujizira kisa kuachwa.kuna sehem lazima uyape maisha nafasi zaidi ya mapenz
 
MAISHA NI HISTORIA INAYOPASWA KUPITIWA KATIKA MATUKIO YA KILA NAMNA....
KUNA MAISHA BAADA YA KILA JAPO.CHA MUHIMU NI KUSAHAU AU KUPUUZIA NA KUSONGA MBELE.
Umesema sahihi mkuu,ila kwa walio wengi ni shughuli pevu mno kulifanikisha hilo.
Jambo ukilipuuzia kamwe halitaigharimu akili.
 
nilipoteza uaminifu moja kwa moja naishi naye ila simuamini tena
 
Things happen for reason.
Ingawa inauma lakini hupaswi kujilaum zaidi kusonga mbele.life goes on.
Haya ni mambo common ambayo nadhani %kubwa wanayapitia.hivyo cha kujiambia kwamba hauko mwenyewe na kama wao waliweza ku give up na maisha yakaendelea why me!unakuta mtu analia na kujizira kisa kuachwa.kuna sehem lazima uyape maisha nafasi zaidi ya mapenz

Bahati mbaya sana wengi tukikutana na wakati mgumu huwa hatutafuti kujua sababu ya hayo kutokea bali ni kujilaumu na kujiona tumepoteza thamani mbele ya jamii.

Kumbe hapana,ni suala tu la kumwomba Mungu kutupa uwezo wa kujua sababu ya hayo yote.
 
Nipo boss,.lazima tujifunze kukubalina na hali halisi ili tuwe salama zaidi.
Yap yap yap.
Kuna wengine hudiriki kujiua aisee kana kwamba maisha bila aliekuwa mwenza hayawezekani kumbe inawezekana tena pengine zaidi ya pale.
Namwomba Mungu anisaidie kama itakuja kutokea kwa upande wangu basi silaha kubwa iwe ni KUPUUZA.
 
Mtangulize Mungu tuu kwa kila jambo,.
 
Niliweka msiba moyoni mwangu, nikalia na kuomboleza, nikamzika kimoyomoyo nikamhesabu hayupo tena duniani nikamtoa moyoni mwangu. Kulipokucha niliamka na furaha mpyaaaa na amani tele kwani hayupo tena akilini na moyoni mwangu. Maisha yanaendelea!
 
Pole kwa msiba mkuu,pia hongera kwa kumzika moyoni na akilini.

Hakika ulivuka kipindi kigumu kirahisi,si wengi wanaweza hivyo kiongozi,narudia hongera sana.
 
Kuumia unapotendwa na unaempenda ni lazima lakini,mwenyezi mungu ameuba kusahau unasahau na maisha yakaendelea ila mie hua namshangaa yule anaeumizwa halafu akaombwa msamaha akakubali yani mie siwezi kwanza hua staki hata kukuona wala kusikia habari zako..
 
Ni kweli, unafanyaje sasa ili yaendelee smoothly?
Toa ushauri wako mkuu ama experience yako kama limeshawahi kukukuta.
kikawaida unatakiwa usi unyime moyo wako amani na furaha kwa ajili ya jambo moja linalo kuumiza kwa kuzingatia yafuatayo
ishi kwa kujua kila jambo hupangwa na mungu na kila kitu hutokea kwa sababu....
accept your past without regreat,
live your present with confidence n
face your future without fear,,, hiyo itakusaidia
pia train your mind to see good in every situation u meet,
jifunze kujisamehe mwenyew kwa kila unalo kosea,,,
acha kuishi maisha ya jana, kumbuka haina nafasi tena katika maisha yako waza kesho njema na yenye tumain
 
Kuumia unapotendwa na unaempenda ni lazima lakini,mwenyezi mungu ameuba kusahau unasahau na maisha yakaendelea ila mie hua namshangaa yule anaeumizwa halafu akaombwa msamaha akakubali yani mie siwezi kwanza hua staki hata kukuona wala kusikia habari zako..
Kumbuka kuwa tunapaswa kusamehe saba mara sabini mkuu.
Kusahau ni jambo jema ila nafikiri kusamehe ni jambo zuri zaidi.
 
Back
Top Bottom