AbasMzeEgyptian
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 407
- 312

SIKU SITA ZILIZOPITA Waziri wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama alikutana na baraza la uwezeshaji wananchi wa Tanzania kiuchumi (NEEC) ambalo majukumu yake ni kuwawezesha wa Tanzania kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira Tanzania. Na Akasisitiza na kutoa amri kuwa serikali ya awamu ya tano ya rais wetu Mpendwa John Pombe Magufuli, PHD inapenda kuona kazi inafanyika kwa vitendo na matokeo yananufaisha wananchi na si vinginevyo.....
Hii vinginevyo aliyosema waziri Mhagama alikuwa akimaanisha kuwawezesha Raia/ Wananchi wa UGANDA (Jana alimteua Raia wa Uganda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF).
Sasa taarifa za uhakika ni kuwa Jenisha sasa anawewesekna na kati ya waTanzania milioni 50 wenye uwezo kashindwa kupata mtu ambaye ni safi na asiye na kashfa ya ufisadi zaidi ya Lawrence Mafuru.
Tukumbuke kuwa huyu huyu Mafuru ametajwa as a "person of interest"na shirika la ujasusi la Marekani FBI kwenye kesi ya uhamishaji wa miamala ya pesa kwenda nje ya nchi (MONEY LAUNDERING) ambayo ilifanywa na benki ya wa Lebanon iliopo hapa nchini ya FBME.
Pia tusisahau kuwa Lawrence Mafuru alifukuzwa kazi NBC na kule BRN alikopelekwa hakufanya lolote lile la maana zaidi ya kashfa za ubadhirifu wa pesa na kumpa mkewe tenda (kama alivyokuwa anafanya yule DG wa TANESCO)
Mafuru alifikia mahala anawalipa mishahara mikubwa na bonus nzuri watu wake ambao aliwapa upendeleo maalum(nepotism) , na kulikuwa na wadada walikuwa ni untouchables ambao inasemekana ni chakula yake (hii nitabia ambayo Mafuru has in common na Magori wa NSSF).
Sasa leo Waziri Jenista Mhagama anamwona Mafuru pamoja na kashfa kem kem za ubadhirifu na ufisadi anamwaona ndio anafaa kuwa bosi mpya NSSF hivi kweli nchi hii hatuna mtu competent wa kuchukua hii post zaidi ya haya magalasa?