Habari za Sabato!
Unajua hii dunia inamambo Sana. Usikubali kushindwa au kuonekana umeshindwa hasa kushindwa kizembe zembe.
Nilisoma humu jamaa mmoja akisema hajawahi kumsikia Paul Makonda akimwaga ung'eng'e. Ile post ilinifanya nicheke Sana. .
Kwa tabia za Makonda ikiwemo kupenda Sifa. Kupenda ligi. Majigambo. Jamaa alikuwa na uhalali wa kujiuliza kwa tabia za Makonda iweje hajawahi kumsikia akimwaga ung'eng'e? Kitu ambacho huenda hata Makonda mwenyewe kinaweza kumsumbua na kwake kuichukulia kama changamoto anayotakiwa kuifanyia kazi.
Sasa ni Leo nimemsikia Makonda akipasua yai akiwa anahojiana na Mchina mmoja kwenye uwanja.😄😄
Amejitahidi lakini bado hana Uhuru kwamba ulimi bado mzito au ana load msamiatina kuinganisha kwa muda kidogo Hali inayomfanya asiwe kwenye fomu 😃 tofauti na angekuwa anaongea Kiswahili.
Je huu ni mwanzo tuu tutegemee mahojiano zaidi ya kingereza kutoka kwa Makonda?
Kwako, unafikiri Makonda angekuwa anajua kingereza kama vile Kiswahili ingekuwaje?
Haya polepole kwenye maoni hapo.
Matusi Leo hayana maana Leo.