Baada ya kusema bye bye ios

Nilikuja humu nikasema bye bye ios na nikaomba ni android gani nzuri na itakayo kaa vizuri na moto pamoja na u quality wa camera.

Nawashukuru sana kwa ushauri wenu na wengi mlinishauri nichukue kampuni ya Redmi.

Kutokana na bajeti yangu niliweza kununua Redmi Note 10, hii simu iko vizuri sana inakaa na chaji, camera safi, iko very faster.

Tatizo langu toka niaze kuitumia nimekuwa na changamoto ya kuumwa kichwa, pamoja na macho sijui shida iko wapi, sijui Display ya hii simu sijui kitu gani.

Nimetumia iPhone miaka yote lakini sikuwahi kupata changamoto kama hii naombeni msaada wenu juu ya hili.

Display yake ni SUPER AMOLED na Display ya iPhone niliyokuwa natumi ni IPS LCD.

Broo jaribu kuzima Bluetooth na wifi. Kuna baadhi ya simu zinaumiza sana. you will thank me
 
Nimeweka Auto brightness na ndo natumia siku zote
Hyo ni issue ya PWM flickering tu. Wewe upo katika lile kundi ambalo mnanotice PWM flickering kirahisi na inawaumiza kichwa. Hata kwenye auto brightness bado unaweza sogeza ile slider isilale sana kwenye low brightness.

Tofauti ya hapo basi badilisha tu simu. Unaweza research zaidi kuhusu issue ya PWM flickering utaona kuwa sio wewe tu ila wapo wengi inaowaumiza pia.
 
Nawaza nirudi tu ios, maana nimekaa nayo muda mrefu na sijaona hizi changamoto. Nimajaribu kufatiria huko google wanasema display ya Amoled pia inachagia kuumiza macho pamoja na kichwa.
 
Angalia hapa:

Kuna watu wengi tu ambao wanakua affected na hii kitu. Wanatakiwa waweke DC dimming kwenye software ila inaonekana kwenye Redmi Note 10 & 10 Pro bado hazina hyo update.

Jaribu kutafuta option ya Anti-flickering kwenye settings
 
Baadhi ya vioo vya OLED vinakua na PWM (Pulse-width modulation) flickering. Vioo vya vya electronic devices vinatumia PWM kucontrol brightness ambapo kinakua kina switch ON and OFF kwa haraka sana. Ssa kuna baadhi ya watu (kama wewe) wanakua wapo sensitive sana na hii ON & OFF kiasi cha kwamba unakua unaona kma display ina cheza cheza. Kwenye OLED ni vigumu kuona display inacheza cheza ila inakua inakuumiza macho na kichwa. Kwenye LCD ndio utaona inacheza cheza. Mara nyingi simu za bei rahisi ndio zinakua na hili tatizo, unakua unaona kma mwanga kwenye kioo unacheza cheza.

Ushauri ni kwamba usipunguze brightness mpka chini au mpaka juu ukiwa unatumia simu ndani au usiku. Tumia brightness ya wastani tu

Kabisa mm huwa naona hivyo sema nikawa nahisi ni baadhi ya simu mbovu,ahsante umenifumbua macho naiona sana hilo tatizo nikitumia Samsung,hata kwenye note 10 plus nilikua na notice hilo
 
Angalia hapa:

Kuna watu wengi tu ambao wanakua affected na hii kitu. Wanatakiwa waweke DC dimming kwenye software ila inaonekana kwenye Redmi Note 10 & 10 Pro bado hazina hyo update.

Jaribu kutafuta option ya Anti-flickering kwenye settings
Unaona hapo mkuu
IMG_20210606_184400.jpg
 
Nawaza nirudi tu ios, maana nimekaa nayo muda mrefu na sijaona hizi changamoto. Nimajaribu kufatiria huko google wanasema display ya Amoled pia inachagia kuumiza macho pamoja na kichwa.
Ukirudi iOS usinunue iPhone yenye OLED/AMOLED display sababu nayo itakuumiza kichwa hvyo hvyo tu. Hapo ina maana iPhone X, XS, XS Max, 11 Pro, 11 Pro Max, na 12 series zote usinunue maana hzo zote zina OLED display na issue ya PWM flickering ipo huko pia.
 
Naona hapo iPhone 7 au 8 na plus zake ndio nzuri kwake. Nina iphone 7 na iphone 8 kwangu naona safi tu ila Samsung note 10 plus imekua pia nikiona kioo kama kinacheza
 
Yeah. Hapo ni kucheza na iPhone 8 kushuka chini, XR na 11 plain. Maana hzo ndio zina LCD na sio OLED
 
Angalia hapa:

Kuna watu wengi tu ambao wanakua affected na hii kitu. Wanatakiwa waweke DC dimming kwenye software ila inaonekana kwenye Redmi Note 10 & 10 Pro bado hazina hyo update.

Jaribu kutafuta option ya Anti-flickering kwenye settings
Mkuu hapo vipi nitakuwa nime solve tatizo?
IMG_20210606_191227.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom