- Thread starter
- #41
Nilipoajiriwa,bosi wangu anamiliki biashara yenye mtaji wa zaidi ya dola Milioni sita au saba hv,ni mtanzania na ana miaka 33,
ana vitega uchumi vingi na vya kutosha,elimu yake ni darasa la saba na si zaidi.........
huyu jamaa amesafiri nchi mbalimbali kibiashara,anaongea kiingereza cha kawaida,ni msomaji mzuri wa jamiiforum ingawa hajajiunga lakini pia anajuai vitu vingi sana vya sasa hv na anaishi kisasa kama vijana wa kisasa.
Nilichojifunza kwa bosi wangu huyu ni kwamba,elimu ni muhimu sana katika maisha,lakini si lazima uwe na elimu kubwa ndo ufanikiwe,mafanikio ni mchanganyiko wa vitu vingi sana,kama kufanya kazi kwa bidii,kusali sana,kuwa na ujasiri wa maamuzi,elimu ya wastani,uelewa wa mambo mengi angalau kidogokidogo,nia ya kufanikiwa na mengine mengi.
sasa mm nasema hv,hao jamaa zako inawabidi wabadilishe mitazamo yao kuhusu maisha huku nyumbani,pia wajifunze wako katika kipindi gani cha kiuchumi na kibiashara,lazima waangalie kuna fursa gani waweze kuzichangamkia,wakichagua kazi wamekwisha...watazeekea nyumbani na mwishowe watakua very frustrated,na hapo kuna hatari ya kuanza kutumia vitu vya ajabu ajabu...wafahamu pia wazazi wao wanaumia sana wakiwaona jinsi walivyo,kusomesha mtu au kumpeleka marekani mtoto si kitu ambacho wazazi wengi wanakimudu ni ghali...tena sana
waambie pia maisha yamebadilika sana siku hz,kuishi au kufanya kazi marekani sio ishu tena,ni kawaida tu,cha muhimu ni noti,noti noti......nasisitiza wasipobadilisha mitizamo yao wataishia pabaya sana huwezi kusema hawawezi kupata kazi wakati kazi zipo zimejaa tele....wawe wabunifu....si lazima aanze na kazi ya kulipwa million mbili....inabidi waanzie chini
maana system imeshawatupa...
Nashukuru sana kwa ushauri mzuri mkuu. Ntafikisha ujumbe!