Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,785
- 21,030
Ikiwa ndugu yako toka nitoke anaweza kukusaliti sababu ya mapito yako ya maisha unastaajabu mtu baki kukuchunia baada ya mapito yakoHellow dears
Ilikuwa morng nipo kwenye mwendokasi kutoka kimara mpaka kivukoni nilushuka pale garden tukawa natembea kuangalia pembeni nikamuona kijana wa kike na wakiume ambao teyali wanaonekana kuchanganyikiwa na madawa ya kulevya wana kiss mbele za watu mimi nikawa natabasamu gafla kaja dem pale naye akawa anacheka
Nika muuliza maswali ya kichokozi baadae tukaachana yeye aliingia NBC mimi nikaingia zangu GSM
Next time tena huyu dada tukakutaba kimara stendi mimi nikamshobokea akasema sikukumbuki nikamkumbusha akafurahi si mnajua mwendokasi wa kimara bila nguvu morng upati siti kidume nikapambana akapata siti na mimi nikasimama
Tulijenga mazoea mpka nikamtongoza akasema yeye anakaribia kuolewa na mchumba wake mwanajeshi nikasema poa tu
Sasa siku mmoja ilikuwa morng tena akasema twende tupate chai tukaingia food point akaniambia nimpe short story yangu nikamwambia anza wewe yake ilikuwa mzuri sana
Mimi kabla ya kumuambia nikamwambia yangu sio mzuri sana akasema sawa ni kweli nikafunguka mpaka akatak kulia kabisa baada ya kutoka pale nikawa nikipiga cm hapokei nikifika stendi ni msubilie hatokei
Siku mmoja nikapewa barua ya kusimamishwa kazi nikamwambia akapiga simu tuliongea mengi sana lakini baada ya hapo mpaka leo hatuna mawasiliano sijajua mpka leo sababu ya yeye kuniacha bila sababu ni ipi
Mimi sio mzuri kwenye uandishi nivumilieni kidogo
Katika maisha jifunze kuweka akiba ya mambo yako, si kila mtu anapaswa kujua undani wako. Kuna watu huogopa madhila ya wengine wakiamini kufunguka kwako kwao ni kutaka msaada.