Baada ya kumkosa kosa jerry muro;waziri Celina Kombani awashukia walimu walevi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kumkosa kosa jerry muro;waziri Celina Kombani awashukia walimu walevi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,062
  Likes Received: 6,838
  Trophy Points: 280
  Kombani awashukia walimu walevi  na Ghisa Abby, Morogoro
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, amewaagiza maofisa wa elimu wa wilaya nchini kuwavua madaraka walimu wakuu wanaoendekeza ulevi na kusababaisha shule zao kufanya vibaya.

  Waziri Kombani alitoa agizo hilo wilayani Ulanga, Morogoro wakati wa ziara ya kukagua shughuli za kimaendeleo jimboni kwake ambapo alipokea taarifa ya wilaya hiyo kuhusu mikakati ya elimu ya mwaka 2010 ili kuinua kiwango cha elimu kutoka asilimia 48.2 ya mwaka 2009 na kufikia asilimia 60 katika kipindi cha mwaka huu.

  Alisema wapo walimu wengi ambao wametoka vyuoni hivi karibuni na wana sifa za ulevi kama walimu wa zamani nao pia wanapaswa kutolewa katika nafazi zao na kupewa walimu wengine wenye sifa nzuri na wanaofuata maadili.

  Akiwakilisha mikakati ya kuinua elimu wilayani humo, Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri hiyo Clemence Mgoano, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2009 walishindwa kufikia malengo ya kuinua taaluma kutokana na sababu mbalimbali.

  Alizitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na utoro wa walimu, ulevi wa kupindukia kwa wakuu wa shule na hivyo kushindwa kuwajibika hali ambayo imesababisha kiwango cha elimu kushindwa kupanda.

  Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka huu, halmashauri hiyo imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuwapatia ushauri nasaha walimu hao pamoja na kutoa barua za kalipio na onyo kwa walimu wakuu walevi, watoro na wanaoshindwa kuwajibika.
   
 2. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwani huyo Waziri alikuwa anamtafuta jerry Muro akamkosa na maemkosa kivipi? tupe ufafanuzi.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,062
  Likes Received: 6,838
  Trophy Points: 280
  ok labda ukuwa na ka idia cha hii kesi
  walipomkamata jerry wamekuta makaratasi ambayo yanaonyesha
  yule aliekuwa mhasibu alikuwa akimtumia pesa kwenye acc na wacha hilo walikuta docs zinzoonyesha mh kombani alinunuliwa magari 2 na huyu bwana so far hata takukuru wanamchunguza nini kimeendelea,......
  wanajiuliza hela alizokuwa akimpa ni za nini???kutoka maktaba inasemekana baada ya mh sana kujua jerrt anataka kumlipua akaamua kumwahi yeye kwenye kesi unayoiona mahakamani.....
  welcome on body
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...