Baada ya kumaliza ya Mh Lema Arusha, Sasa twendeni Lindi na Kilombero

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,733
239,339
Wakuu , natanguliza salamu.

Haki siku zote hudaiwa , hailetwi kama mvua kutoka mawinguni , katika nchi yoyote yenye ukandamizaji wa haki kama ilivyo Tanzania , njia pekee ya kuipigania haki ni mapambano ya kisheria.

Suleiman Methew , mtu aliyelitumikia Taifa hili na kuliletea heshima kubwa katika soka , leo hii anatumikia kifungo cha uonevu kabisa , kutokana na chuki ya kisiasa kutoka kwa watu wachovu na waoga ambao hawakuwahi kuifanyia lolote nchi hii , kesi ile ni nyepesi mno ! Zaidi ya kinachoitwa Maagizo kutoka juu hakuna mahali popote Methew anapoweza kufungwa .

Mh Lijuakali ni kijana anayefahamika kwa uwezo wake wa kujieleza mbele ya umma , kupigania haki na kuelimisha umma kuzijua na kudai haki zao , yaliyotokea Morogoro wakati wa Uchaguzi mkuu 2015 yanafahamika , " kubadili mawe kuwa mikate " haikuwa kazi rahisi , amefungwa kwa chuki za watawala , wala hakufanya kosa la kufungwa kifungo kile .

TWENDENI TUKAWAPIGANIE ILI WARUDI KUWA HURU KAMA SHERIA INAVYOTAMKA .

Nakala imfikie Tundu Lissu .
 
Naona LEMA amekutoa mafichoni leo.

KWANI IMEISHA AU NI DHAMANA TUU, KESI HATA HAIJAANZA, LEMA HAPO KAFUNDISHWA TUU ADABU , YAAAN MIEZI MINNE NA BADO KESI HAIJAANZA, ALAFU UNASEMA TUMEMALIZA DU??? ACHA KUJIPA
 
KWANI IMEISHA AU NI DHAMANA TUU, KESI HATA HAIJAANZA, LEMA HAPO KAFUNDISHWA TUU ADABU , YAAAN MIEZI MINNE NA BADO KESI HAIJAANZA, ALAFU UNASEMA TUMEMALIZA DU??? ACHA KUJIPA
Huitaji kuwa mtabiri kujua kati ya lema na mkewe, mmoja ataenda ,"nyea debe"....time will tell....
 
Kabisa haki ya MTU aipotei inacheleweshwa tu makamanda ni wengi Mungu asaidie tuwapiganie wote makamanda wetu
 
Atanyooka sasa, atakuwa mpole kama kuku aliyenyeshewa na mvua. Chezea JPM weye!
 
Kilombero tunakuja
e549b35d341e87fbb1493dab902f310f.jpg
 
Unaandika uongo kwa faida ya nani ?
Ukifanya " tafakari huru, macho mbele usawa wa kati"....hiyo ndio picha inayokuja....
Huenda isikufurahishe, kama itakavyokuwa kwa wafuasi wake wengi na wanachama wenzie ktk chama chake...
...wengine tutasikitika tu kama tunavyosikitika likijiri jambo la kusikitisha....ni mwakilishi wa umma lemma, hatusahau kweli hii....
 
Yule DPP Msukuma ana uwezo mdogo san tutawashinda mahakamani kiurahisi sana ! Njama zote za kishamba tumezibaini kizembe sana .
 
Back
Top Bottom