Baada ya kukusanya korosho na kuzirudisha, naomba kujua serikali imepata hasara kiasi gani

Tunajua hili sakata la korosho halikuwaacha wakulima peke yao salama, hata serikali nayo imeingiza hasara kubwa sana.

Gharama zilizotumika kusomba korosho, gharama za kuzitunza, kuhesabu, kulipa posho wanajeshi na ma officers.

Hii ni hasara kwetu walipa kodi wazalendo. Na kama mzalendo hii hasara inaniuma sana. Tunahitaji kujua ni kiasi gani na mamlaka husika iliyosababisha hii hasara inawajibishwaje kama walivyowajibishwa watumishi na viongozi mbali mbali.

Bila kumsahau yule waziri alyetumbuliwa kisa korosho.

Sent using Jamii Forums mobile app

Malipo ya Dhulma hayana faida.
 
Back
Top Bottom