Baada ya kujitathimi nimegundua haya

souljar

JF-Expert Member
Feb 16, 2021
592
1,000
Habari wanaJF, kwa wale waliopitia post yangu iliyopita baada ya kupata mvunjiko wa moyo nimekaa chini na kugundua baadhi ya makosa niliyoyapuuzia, haya yanawezwa kufanywa na yoyote liwe kama angalizi kwa vijana.

1)KUWA NA JIKO BAR
Katika kitu nilichopuuzia ni huyu binti kuwa na jiko bar na nikajiuliza mwanzoni imekaaje ilo sema baada yakusikia kwake inafaida na nikitu nimemkuta anafanya nikasema twende kazi lakini kiukweli kuna mengi sana nyuma la ilo.

2)KUWA SINGLE MOTHER
Nalo sikupata mda wakuliangalia kwa upana lakini nilijiuliza maswali kuwa na urembo wote jamaa kakimbia kuna jambo hapa sema kutokana na kujieleza kwake kuwa jamaa alikuwa mzinguaji na wamegombana vibaya na alimfata akakuta anamwanamke mwingine inasemekana kaoa so nikasema inatosha twende kazi

3)KUPENDA SANA
Hapa napo nadhani nilichapia kuonyesha kumpenda sana mbele za ndugu zake na yeye mwenye kila jambo kwangu ndio tu.

4)KUTOA HELA KILA AKIITAJI
Hapa napo ilikuwa tatizo nililokuja kuona maana hakuna nililokataa wala kusema sina nitafanya nifanyavo kutimiza kwa iyo miezi 7 nimekata over 10M, haipiti siku mbili bila kutuma laki au elfu 50 ndani ya week ukiacha matumizi mengine saloo,kodi na vingine

5)KUTAMBULISWA NYUMBA
Hili lilinifanya nitoe guard zangu kabsa kuamini nime conquer tayari,mzee ananijua, mtoto na ndugu,bila kujiuliza kuwa mimi sio wakwanza kupelekwa pale.

6)MYWAJI POMBE
Jingine ambalo sikulitilia mkazo ni mnywaji mzuri tu wapombe na anakichwa kizuri kwenye pombe nikajiuliza inakuwaje kwa wengine kama iko ivi maana yake si easy go sema akasema anakunywa akiwa na mimi ivo.

7)HATAKI KUULIZWA KITU
Kitu kingine nilichoingia mkenge ni kwenye kuuliza jambo kuwa ameonekana sehemu basi ni ugomvi mkubwa sana mpaka kutopokea simu siku kadhaa eti namambo ya kitoto nisimuulize ujinga..

8)KUWA NA AHADI NYINGI
Kosa Jingine ni kwakuwa huyu binti alikuwa anataka vitu vingi nilibidi niwe mtu wakuweka ahadi kwa kujua vingine naweza vingine siwezi lakini acha nimeidhishe kwa kusema sawa tutafanya.

9)KUKUBALIANA NA KILA ANALOTAKA
Hapo nako nilikosea sana kwenda naye kwa YES kwa kila jambo analotaka na kuomba kwangu ilifika mda ilinibidi nimkudishie gari miezi mitatu

10)KUJIFICHA KWENYE DINI
Hapa napo aliniweza kwa kuniaminisha ni mpenda dini na anahofu ya Mungu lakini matendo yalikuwa yanaenda against na matakwa ya Mwenyezi sijui anaabudu nini namuachia mwenyewe ilo.

:-Baada ya kuacknowledge hayo napenda kusema MAPENZI NI UGONJWA WA AKILI, VIJANA TUJENGE TAIFA SASA.


Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 

Niwaheri

JF-Expert Member
May 2, 2020
936
1,000
Nadhani sasa umekubali matokeo na hautorudia kosa,umakini katika kila jambo unahitajika
Leo hyu anaweza akakuchezesha sindimba na baada ya mda ukakutana na mwingine mambo yakawa hivohivo kikubwa tuache mihemko,ukishajua ni nini unakitaka wala hautojuta
 

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
13,456
2,000
Bila shaka mtoa mada,
Umetudhihirishia jins gan ulkua mtanzania mzarendo na MNYONGE kwerikweri
IMG_20210402_160935.jpg
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,197
2,000
Alikuwa sahihi kukwambia una mambo ya kitoto na kukuonya usimuulize ujinga. Mengine yote ni matokeo ya kupuuza ushauri wake huo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom