Baada ya Kudumaa, Huenda Samia Ikaipeleka Nchi Kileleni

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Kuna wakati, tangu wakati wa kupigania uhuru, Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa zina mvuto wa pekee kwenye siasa za kimataifa. Huo ulikuwa ni wakati wa Rais Nyerere. Ni nyakati hizo ndipo Tanzania ilikuwa Mwenyekiti pekee wa nchi zilizo mstari wa mbele kupigania ukombozi kusini mwa Afrika. Kila nchi iliyopata uhuru, viongozi wake walitoa heshima ya pekee kwa Tanzania. Afrika Kusini, mara baada ya Mandela kuwa Rais, mpaka walifikia kuruhusu mazao ya Tanzania yaingie Afrika Kusini bila ya kodi yoyote. Ni bahati mbaya tulishindwa kuitumia nafasi hiyo kwa sababu uzalishaji wetu ni duni.

Hata katika Afrika Mashariki, pamoja na kutokuwa na demokrasia kamili, Tanzania ilitazamwa kama nchi ya afadhali kwenye demokrasia.

Hata katika siasa za kimataifa, Tanzania kupitia Mwalimu Nyerere, ilikuwa ina heshima yake kutokana na misimamo thabiti kwa mambo iliyoyaamini kuwa ni sahihi.

Baadaye tukapotea kidogo, na baadaye tukapotea zaidi, mpaka kukaribia kuwa miongoni mwa nchi vinara wa kuua demokrasia, kukanyaga haki za watu, kugandamiza uhuru wa maoni wa watu na uhuru wa vyombo vya habari. Bila hata ya kutafuta reference, hata kwa Afrika Mashariki, tukawa Taifa duni. Na katika haki, demokrasia na kuheshimu uhuru, Kenya iliweza kupanda na kuchukua nafasi ambayo ilikuwa nayo Tanzania.

Hakuna baya linalodumu milele.

Kuingia kwa Rais Samia, kukaanza kuleta unafuu. Hatua kwa hatua, kuna mambo yakawa yanabadilika positively kwenye upande wa utawala bora japo katiba iliendelea kuwa ile ile yenye mapungufu mengi. Na wa kupaza sauti hatukuacha, tukimtaka Rais afanye zaidi, aende kwenye msingi, aende kwenye shina badala ya kupurua matawi.

Nimesoma hotuba ya Rais Samia ya leo kwa viongozi wa vyama vya siasa. Hakika, bila unafiki, wala chuki, wala upendeleo, ni hotuba fupi lakini iliyo nzuri kwa sababu iligusa upungufu wa msingi wetu, KATIBA, lakini kubwa zaidi ni juu ya namna njema anayoifikiria katika kuifikia. Kama atayaishi maneno yake, hakika Tanzania inaenda kupaa na kuwa kinara katika utawala bora, na hasa kutokana namna tutakavyoipata katiba mpya.

Nchi nyingi, pamoja na jirani zetu Kenya, wamefika walipofika kwa umwagaji mkubwa wa damu. Kama sisi tutaipata katiba mpya nzuri, iliyopatikana kwa njia shirikishi, tena ikapatikana katika maelewano, umoja na upendo, tutakuwa miongoni mwa mataifa machache sana Duniani.

Mwalimu Nyerere, tofauti na mataifa mengi Dunia, alifanikisha Tanzania kupata uhuru wake bila ya umwagaji damu. Mungu amsaidie na amwongoze Rais Samia, tupate katiba mpya isiyo na jalada la damu ya Mtanzania yeyote. Rais Samia, akilifanikisha hilo, hakika baraka juu yake, na heshima ya Watanzania kwake, atadumu nazo milele, awe katika Ulimwengu huu au hata baada ya maisha yake ya hapa Duniani.

Tunataka tuipate katiba mpya nzuri, kila mmoja, isipokuwa kwa mapenzi ya Mungu, aishi katika katiba hiyo. Yatufaa nini kupata katiba mpya huku wenzetu wengine wakiwa vilema au wamepoteza maisha yao?

Kwa shughuli za vyama vya siasa, japo Rais amegusia, nasi tunasisitiza, Askari, hasa jeshi la Polisi linahitaji mafunzo maalum ili liweze kubadilika, liwe na weledi mkubwa lakini weledi unaozingatia haki za watu, na lijitenge kabisa na shughuli za vyama vya siasa, libakie kuwa msimamizi wa amani badala ya kutumika kuvuruga amani wakati wa shughuli za vyama vya siasa.

Kama Rais Samia atasimama katika maneno yake, hakika mwaka 2023, utakuwa mwaka wa kukumbukwa kwa mema mengi, kubwa kuliko yote, kuweza kutengeneza mwongozo mkuu wa Taifa letu.

Roho wa Mungu asaidie, Rais Samia azungukwe na washauri wenye dhamira njema kwa Taifa letu, na wale wanafiki wakapeperushiwe mbali ili Taifa lipate kupona.

Tunapoelekea kwenye dhamira ya Rais, dhamira ya kupata Katiba mpya, tujitahidi kuziangalia hoja, michango na contents zake, tusiangalie aliyetoa ametoka chama gani, ni wa dini gani, wa kanda gani au kabila gani. Kila mmoja aamini na aone kuwa Katiba nzuri ni kwaajili ya kila mmoja, ni kwaajili ya Taifa zima.

Mod: tafadhali rekebisha hiyo heading, badala ya kusomeka 'ikaipeleka' isomeke, 'akaipeleka'
 
Katiba mpya siyo muarobaini wa matatizo yetu ya kutokuendelea, maradhi, ujinga, umaskini, elimu, barabara etc.
Kenya wana katiba mpya lakini umaskini umeongezeka, kura bado zinaibiwa, kwa kifupi katiba mpya haijawasaidia
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Bavicha ni wepesi sana aisee!

Kwa kipi sasa? Yani mtu akunyanganye hela zako alafu akikurudishia uanze kushangilia na kumuona shujaa?

Huu ni utaahira kabisa!
 
Mataga leo utateseka sana, huamini kama legacy inazidi kuporomoka tu[emoji16]

Ni maamuzi gani ambayo unaona yanabadili maisha ya watu huyo Samia kafanya???
 
Back
Top Bottom