Baada ya Kikwete kukaribia kufika mwisho basi kila mtu anadhani anaweza kuwa Rais

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Naweza kusema watu wengi sana hawakuamini kama Kikwete angeweza kumaliza msimu wake wa miaka mitano ya mwisho bila ya mambo kukwamia njiani. Kikwete alioneekana ni kiongozi dhaifu sana, asiye na maamuzi wala uwezo wa kuifikisha nchi popote. Wengi walidhani uwezo wa Kikwete aliokuwa nao wakati anaanza kuongoza nchi ulitokana na nguvu ya Lowassa. Lakini baada ya Lowassa kuondolewa wakaamini kwamba Kikwete asingefika kokote. Kitendo cha kuona Kikwete anakaribia kumaliza ungwe yake bila kukutana na changamoto yoyote ambayo ni tishio kubwa kwa nchi, basi kila mtu, hata wale wasio na uwezo hata wa kuongoza nyumba kumi hivi sasa wanajiona kwamba wanaweza kuwa marais.

Just kwa kujua kwamba Kikwete alikuwa Rais dhaifu lakini ameifikisha nchi mwisho wa safari, basi wanaamini yeyote yule anaweza kuwa Rais. Ni ulimbukeni kukaa chini na kuufikiria Urais, ilihali kwenye nafasi za ubunge tu mmeboronga. Wengine kati ya wanaotangaza kutaka urais tayari walishaitwa mawaziri mizigo, nashangaa sana waziri mzigo anapotafuta urais. Anataka kuwa rais mzigo au ndiyo kusemaje? Kuna wengine wenu mnayetangaza kutaka urais hata bungeni hamuwezi kurudi msimu ujao, halafu mnafikiria urais! Bora mtulie tu mfanye yanayoendana na uwezo wenu. Urais si cheo cha kushikwa na kila mtu bwana.
 
Kwani katiba ya nchi inasemaje mtu kwa raisi au athari za mazingira yanayotuzunguka na familia tulizotoka ndo tunaweka limitation ya mafanikio ya mtu kama wewe unaona huwezi kuwa raisi sio kila mtu awezi
 
Kikwete Hajawahi kuwa Rais Dhaifu Labda kwa Wenye Udhaifu wa Kufikiri
 
Urais una ugumu gani? Kuzurura ughaibuni, kuombaomba, kuchekacheka, kubembea ughaibuni, kulalamika kwa wananchi unavyopotoshwa, kuhudhuria matamasha/misiba/harusi/kutembelea wagonjwa.
Hata mimi mwalimu wa UPE naweza
 
Urais una ugumu gani? Kuzurura ughaibuni, kuombaomba, kuchekacheka, kubembea ughaibuni, kulalamika kwa wananchi unavyopotoshwa, kuhudhuria matamasha/misiba/harusi/kutembelea wagonjwa.
Hata mimi mwalimu wa UPE naweza
Na hii ndiyo tafsiri ya urais kwa wengi, ndiyo maana kila mtu anadhani anaweza.
 
Back
Top Bottom