Elections 2010 Baada ya kazi ngumu...

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Ndugu zangu wote mliopenda na kutamani kuiona Tanzania mpya, nawapa hongera kwa kazi nzuri sana ngumu ambayo mmeifanya.

Nimepokea huu ujumbe mzuri na naamini utawafaa katika kipindi hiki ambacho tunajipanga upya kurudi katika uwanja wa mapambano.

Wapendwa wangu na wana mapambano ya kuikomboa TZ.
Ninalazimika kuandika kwa ufupi sana.Ninajua na kufahamu fika kuwa kazi yenu haikuwa ndogo na matunda yake hata baada ya uchakachuaji yameonekana. Pamoja na matamko tunayoyasubiri, bado hatuna sababu ya kukata tamaa. Safari ya Ukombozi mara zote ni ngumu, inayochosha na wakati mwingine kukatisha tamaa. Kukata tamaa ni dhambi kubwa.
Tunasubiri jeshi lililotumwa Dodoma liingie kazini.
Tunawaomba wana mapambano wote, viongozi wote, wana mtandao na marafiki wa DR.Makini kusisitiza kuwa na umoja na mshikamano. Graph imepanda, kila mmoja anashangaa, jipeni moyo. Safari ya ukombozi wa TZ bado ni ndefu.
Tunahitaji kusimama imara dhidi ya sauti za vitisho. Mwisho wa Uchaguzi ni mwanzo wa Uchaguzi mwingine.
Kujipanga mapema ni vizuri zaidi.
Leo, bei za mafuta zimepanda....ni machache tu....
Steve Biko alisema "I write what I like...".Kwangu sitanyamaza, nitaendeleza mapambano kumkomboa mtanzania....wewe je? Msalimie mwana mapambano na mpambanaji mwingine.
 
Back
Top Bottom