Schoolface
Senior Member
- May 7, 2021
- 156
- 165
Habari
Nimekua na muda mrefu sana pasipo kuhudhuria Misa takatifu ya roman Catholic kulingana na shughuli mbalimbali ambazo nimekua nafanya pengine kukosa muda wa kwenda kanisani kutokana na uchovu wa kazi au mambo mengi ya kidunia.
Lakini baada ya Jana kukaa na kutafakari mambo mengi nikasikia sauti inaniambia kesho ni lazima uende kanisani basi baada ya mapumziko ya ijumaa mosi ilipofika jioni nikasema basi niandae nguo ili kesho niweze kwenda kanisani na ilipofika alfajiri ya Leo nikaamka mapema sana nikajiandaa kwajili ya kwenda kanisani basi nikafanikiwa kufika salama na nilipo fika Ile naingia kwenye mlango wa kanisa nikahisi Kuna kitu kimenivaa na nikajiisi amani sana ambayo nimeikosa kwa muda mwingi sana basi nikasali vizuri mpaka Misa ilivyo Isha.
Nimetoka najisikia vizuri sana pamoja na mambo mengi ninayo pitia pamoja na mawazo lakini Leo kwa mara ya kwanza nimejihisi mtu mwenye amani sana sijui imesababishwa nanini lakini wakuu nahisi Kuna upako uko katika ndani ya moyo wangu hii amani na utulivu nilioupata sikumbuki mara ya mwisho nimeupata lini wakuu tumkumbuke Mwenyezi Mungu Kila mtu katika Imani yake usisahau kwenda kumuomba mwenyezi Mungu na kuanzia Leo naapa kutokukosa kushiriki Misa takatifu.
Niwatakie ijumaapili njema na yenye baraka Ameeeee.