Baada ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kusema hawatavunja mashine za kujifukiza, Kigwangalla ahoji zaidi...

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,876
MASWALI YANGU KWA MSEMAJI WA MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL!
———————————
Hamisi Kigwangalla, MD.

Nimefarijika kwamba msemaji wa Muhimbili amejitokeza na kueleza kuwa Kuna utafiti unaoendelea juu ya nyungu pale MNH. Ni kitu kizuri.

Kwa ajili ya uelewa wa pamoja ningependa kujua mambo yafuatayo:

- Utafiti unaofanyika ni wa aina gani? Study design? Ni utafiti wa kutaka kujua kama nyungu ni tiba sahihi ya COVID-19 ama la?

- Kama jibu la swali la kwanza ni ndiyo, basi ni Utafiti wa ‘Clinical Trial’ ama ni nini? Kama ni Clinical Trial atusaidie kutujulisha juu ya:

- Malengo ya utafiti ni nini?

- hypothesis ya utafiti wao ni nini?

- Sample size

- Sampling frame

- Sifa za cases na sifa za controls, na atuambie namna wanavyopatikana na Kama Kuna ‘blinding’ ama la! Na je, ni single blinding and double blinding?

- Atuambie Principal Investigator (PI) wa hiyo study ni nani? Ana sifa (CV) gani?

- Amepata Ethical Clearance kutoka wapi? Na Je, wana kibali cha COSTECH cha kufanya utafiti huo?

- je, hao subjects waliofanyiwa utafiti, wanawafuatiliaje ili kujua matokeo?

- Dawa inayowekwa mule, dozi yake ni kiasi gani? Inapimwaje? Hiyo mitishamba inayowekwa humo ina ‘active ingredient’ gani? Ina side effects gani? Imepitia hatua gani mpaka kuonekana kuwa inaweza kutumiwa na binadamu?

- Utafiti utakamilika lini?

===

Muhimbili Wamjibu Kigwangalla ‘Hatuondoi Nyungu Muhimbili’


Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema haitaondoa huduma ya kujifukiza Hospitalini hapo kama ilivyoshauriwa na Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla, kwakuwa iko kwenye utekelezaji sahihi wa majukumu yake ya kitafiti kama wanavyofanya Wanasayansi wengine kote Duniani.

Taarifa iliyotolewa leo na Aminiel Aligaesha, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH imesema———“kuna ujumbe wa sauti ya Mbunge Kigwangalla unaosambaa kwenye mitandaoni ambao pamoja na mambo mengine anataka huduma ya kujifukiza iliyoanzishwa Muhimbili kuvunjwa kwa kuwa inaleta picha mbaya, Covid 19 ni ugonjwa mpya ambao hadi sasa Duniani hakuna mwenye majibu sahihi, majibu sahihi yanatokana na tafiti zinazofanywa sehemu mbalimbali”

“Kwa muda kumekuwa na taarifa kuwa tiba asilia ikiwemo kujifukiza kunasaidia katika tiba ya Covid 19, tafiti mbalimbali kutoka sehemu nyingine Duniani kama Israel na Italia zimeongelea kujifukiza (steam therapy) kama njia mojawapo ya tiba ya ugonjwa huu na mengine ya upumuaji, MNH iliona kuna umuhimu wa kuleta huduma hii ili Wananchi walio tayari waitumie na pia Wataalamu wapate nafasi ya kuifanyia utafiti kwa njia za kisayansi na kutoa majibu sahihi kama inafaa au haifai”———MNH

“Hii itatoa nafasi kwa Wataalamu wetu kuwa sehemu ya mjadala wa tiba ya Covid 19 badala ya kusubiri kila wazo au jibu kutoka kwa wenzetu, na hii pia inawakumbusha Wataalamu wetu wawe tayari kufanya utafiti na kuchangia kutoa majibu yanayohitajika badala ya kusubiri kila kitu tufanyiwe na kuletewa mezani”———MNH

”Mpaka sasa zaidi ya Wananchi 1,100 wakiwemo Wataalamu wa Afya (Madaktari, Wauguzi n.k) waliotumia huduma hii wametoa taarifa ya kuridhishwa na huduma hii”———MNH

Zaidi, soma: Dkt. Kigwangalla: Mashine ya nyungu iliyo Muhimbili ivunjwe, viongozi wavae barakoa
 


"Conclusions: Our work suggests that several herbal medicines have safety margins superior to those of reference drugs and enough levels of evidence to start a clinical discussion about their potential use as adjuvants in the treatment of early/mild common flu in otherwise healthy adults within the context of COVID-19. While these herbal medicines will not cure or prevent the flu, they may both improve general patient well-being and offer them an opportunity to personalize the therapeutic approaches."

"Steam inhalation and hot fomentation (with aromatic oils such as menthol) provide satisfactory clinical relief in nasal and throat congestion, bronchoconstriction, headache, and sinusitis. Its role in improving nasal conditioning, improving nasal mucus velocity, and reducing congestion and inflammation has been reported in several clinical studies"

 
Kwani wanapaswa kumjibu mtu au hoja iliyowekwa mezani ?

Tukianza kuwa na tabia ya kujibu / kusikilizwa kilichosemwa na sio nani kasema tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana kama taifa...

Even a Broken Clock is Right Twice a Day...
umeongea jambo la maana sana, huwenda hata kigwa ameongea hoja zake kuna kitu amekiona mfano vifo vingi vya watu
 
Back
Top Bottom