Baada ya 'battle' kati ya Spika Ndugai vs CAG na Masele vs Ndugai, sasa ni Makonda vs Ndugai

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amemjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufuatia kauli aliyoitoa leo mbele ya Rais Dkt. John Magufuli, akiwalalamikia Wabunge kuwa wameidhihaki timu ya Taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) baada ya kupigwa bao 2-0 na Senegal juzi kwnye michuano ya AFCON.

Spika amesema kauli ile ni sawa na kumdanganya Rais hadharani kwani wabunge wanaiunga mkono Taifa Stars kwa asilimia mia moja na kauli aliyoitoa ya kusema Taifa Stars wanahitaji lishe hakuwa na maana ya kuwatusi ama kuwabeza.

Awali, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliomba mwongozo wa spika kuhusu suala hilo; “Mmoja ya viongozi amewabagaza wabunge tena mbele ya Mkuu wa nchi, tunapaswa tupate mwongozo wako Spika, kwa sababu anaweza kutokea mwingine akalisema bunge na asifanywe chochote, tunakufahamu hupendi bunge hili kuchezewa, kutomaswatomaswa wala kudharauliwa, nini kimekupata leo unajitetea? Tunaomba usimame utoe kauli kama spika wa bunge na mkuu wa mhimili huu.”

Akizungumzia suala hilo, Spika Ndugai amesema; “Tusilikuze sana jambo hili, kama wabunge wangekuwa na mawazo ya kuidhihaki timu yetu je, kungekuwa na wabunge wengine 30, wanaondoka kesho kwenda kwenye mchezo mwingine wa Taifa Stars?

“Haya ni mawazo ya mtu mmoja ambaye bahati mbaya ndo hivyo, kuna viongozi wa Serikali ambao wana diriki kumdanganya Rais hadharani, kiongozi wa Serikali unapoongea mbele ya Rais jipangee, sio unawasingizia wabunge wamekukosea nini?
amesema Ndugai

“Natamani ningefunguka kidogo kuhusu…. lakini inatosha. Nasema wazi mbele ya Mwenyezi Mungu, bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi, na kwa sababu ana nguvu aliyo nayo na makundi kwenye mitandao ya kijamii, anaweza kumtukana Spika, si vizuri kufanya hivyo. Kama kuna mtu ana deni la kufanya kwa Taifa Stars ni yeye, akitaka niseme nitasema, kwa leo imetosha,” amesema Spika Ndugai.

“Leo mchana, RC Paul Makonda wakati akizungumza mbele ya Rais Magufuli wakati akizindua Ghala na Mitambo ya Kuchakata Gesi ya LPG ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited katika eneo la Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam alisema;

“Mimi ni mpenzi mkubwa wa Taifa Stars na nimeumizwa sana na matokeo ya Senegal, lakini kilichoniuma kikubwa zaidi ni watu kuwabeza wachezaji wa Taifa Stars ambao wameipa heshima nchi hii kwa miaka 39 kuingia AFCON 2019, leo wameonekana hawana afya njema, hawana chochote, hawana uongozi mzuri, hatuwezi kuwa na taifa la namna hii.

“Mheshimiwa Rais, kama itakupendeza ninaomba unipe ruhusa niende Misri kuwapa hamasa vijana wetu, nina uhakika watashinda mechi ijayo dhidi ya ndugu zetu Kenya. Vijana wetu wana ari kubwa ya ushindi, hata leo asubuhi nimeongea na nahodha Mbwana Samatta, amenihakikishia wapo vizuri na watashinda mechi ijayo,” alisema Makonda.

MAONI: KUMBE NDUGAI KUNA BAADHI YA WATU ANAWAOGOPA, ANAONGEA KWA KUJITETEA BADALA YA KUMWITA KWENYE KAMATI YA MAADILI. AKIKATAA ANALETWA KWA PINGU.
Kauli ya spika ya kusema kuwa anatamani angefunguka zaidi inaacha maswali mengi kuliko majibu, huenda kuna zile siri kuuu za... alitaka kuzitoboa.

Pia akumbuke baada ya kumgusa first born, kifuatacho ITV ni kumgusa mzazi na hatimaye atatoweka kwenye ramani ya siasa.

Namkumbusha kuwa kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu, utatumika sana na mwisho umuhimu wako ukiisha unatemwa kama BIG G

Makonda yuko sahihi....
Huyo anaejiona eti ni mzalendo bora akae kimya...na hao wabunge wasiende....
Pia kumbukeni,,,wabunge wameenda kutoa hamasa
Serkali pia imeenda kutoa hamasa kupitia Mkuu wa Mkoa mwenye akili nyingi na mbunifu ambae anapigwa vita na wahuni,,,ndugu Paulo Makonda...
 
Spika wa Bunge, Job Ndugai, amemjibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufuatia kauli aliyoitoa leo mbele ya Rais Dkt. John Magufuli, akiwalalamikia Wabunge kuwa wameidhihaki timu ya Taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) baada ya kupigwa bao 2-0 na Senegal juzi kwnye michuano ya AFCON.

Spika amesema kauli ile ni sawa na kumdanganya Rais hadharani kwani wabunge wanaiunga mkono Taifa Stars kwa asilimia mia moja na kauli aliyoitoa ya kusema Taifa Stars wanahitaji lishe hakuwa na maana ya kuwatusi ama kuwabeza.

Awali, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliomba mwongozo wa spika kuhusu suala hilo; “Mmoja ya viongozi amewabagaza wabunge tena mbele ya Mkuu wa nchi, tunapaswa tupate mwongozo wako Spika, kwa sababu anaweza kutokea mwingine akalisema bunge na asifanywe chochote, tunakufahamu hupendi bunge hili kuchezewa, kutomaswatomaswa wala kudharauliwa, nini kimekupata leo unajitetea? Tunaomba usimame utoe kauli kama spika wa bunge na mkuu wa mhimili huu.”

Akizungumzia suala hilo, Spika Ndugai amesema; “Tusilikuze sana jambo hili, kama wabunge wangekuwa na mawazo ya kuidhihaki timu yetu je, kungekuwa na wabunge wengine 30, wanaondoka kesho kwenda kwenye mchezo mwingine wa Taifa Stars?

“Haya ni mawazo ya mtu mmoja ambaye bahati mbaya ndo hivyo, kuna viongozi wa Serikali ambao wana diriki kumdanganya Rais hadharani, kiongozi wa Serikali unapoongea mbele ya Rais jipangee, sio unawasingizia wabunge wamekukosea nini?
amesema Ndugai

“Natamani ningefunguka kidogo kuhusu…. lakini inatosha. Nasema wazi mbele ya Mwenyezi Mungu, bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi, na kwa sababu ana nguvu aliyo nayo na makundi kwenye mitandao ya kijamii, anaweza kumtukana Spika, si vizuri kufanya hivyo. Kama kuna mtu ana deni la kufanya kwa Taifa Stars ni yeye, akitaka niseme nitasema, kwa leo imetosha,” amesema Spika Ndugai.

“Leo mchana, RC Paul Makonda wakati akizungumza mbele ya Rais Magufuli wakati akizindua Ghala na Mitambo ya Kuchakata Gesi ya LPG ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited katika eneo la Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam alisema;

“Mimi ni mpenzi mkubwa wa Taifa Stars na nimeumizwa sana na matokeo ya Senegal, lakini kilichoniuma kikubwa zaidi ni watu kuwabeza wachezaji wa Taifa Stars ambao wameipa heshima nchi hii kwa miaka 39 kuingia AFCON 2019, leo wameonekana hawana afya njema, hawana chochote, hawana uongozi mzuri, hatuwezi kuwa na taifa la namna hii.

“Mheshimiwa Rais, kama itakupendeza ninaomba unipe ruhusa niende Misri kuwapa hamasa vijana wetu, nina uhakika watashinda mechi ijayo dhidi ya ndugu zetu Kenya. Vijana wetu wana ari kubwa ya ushindi, hata leo asubuhi nimeongea na nahodha Mbwana Samatta, amenihakikishia wapo vizuri na watashinda mechi ijayo,” alisema Makonda.

MAONI: KUMBE NDUGAI KUNA BAADHI YA WATU ANAWAOGOPA, ANAONGEA KWA KUJITETEA BADALA YA KUMWITA KWENYE KAMATI YA MAADILI. AKIKATAA ANALETWA KWA PINGU.

Zitto mbona ana misamiati ya ajabu ajabu kama zwazwa, bagazwa, sijui ipo kwenye kamusi ya Kiswahili?
 
dhaifuz vs poyoyoz
 
Makonda yuko sahihi....
Huyo anaejiona eti ni mzalendo bora akae kimya...na hao wabunge wasiende....
Pia kumbukeni,,,wabunge wameenda kutoa hamasa
Serkali pia imeenda kutoa hamasa kupitia Mkuu wa Mkoa mwenye akili nyingi na mbunifu ambae anapigwa vita na wahuni,,,ndugu Paulo Makonda...

Hawa ndio vijana wake aliowanena Spika Ndugai.
 
Makonda yuko sahihi....
Huyo anaejiona eti ni mzalendo bora akae kimya...na hao wabunge wasiende....
Pia kumbukeni,,,wabunge wameenda kutoa hamasa
Serkali pia imeenda kutoa hamasa kupitia Mkuu wa Mkoa mwenye akili nyingi na mbunifu ambae anapigwa vita na wahuni,,,ndugu Paulo Makonda...
Ungeandika na namba zako za simu ili makonda akusajili
 
Back
Top Bottom