Baada ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa kumaliza muda wake, mtu sahihi wa kumrithi alitakiwa awe Magufuli. Nchi ingepaa sana

Kwani yeye ni kutoka chama gani hapa nchini?
 
Mkuu unafikiri ni akili za kijamaa? Incompetency yake ndo inamfanya aamini kuwa akitembelea kivuli Cha Nyerere labda ataonekana yeye ni bora,yaani hata wakati aliopo haujui
Ila hicho kivuli cha nyerere ndio kimejenga na kumalia hospitali ya rufaa mkoani mara iliyosimama tika mwaka 1986.

Kivuli cha nyerere ndio kimehamishia makao makuu dodoma plan ya mwaka 1974.

Kivuli cha nyerere ndio kinajenga mradi wa stieglers gorge ambao plani yake ni ya mwaka 1969.

Kivuli cha nyerere ndio kimeifanya dar es salaam iwe kwenye top ten ya majiji yanayokuwa kwa kasi africa kutokana na miradi ya kimkakati na miundo mbinu ya kisasa zikiwemo
Streets lights and street roads.
Barabara za kisasa kama mwenge morocco, ubungo chalinze.
Tanzanite bridge & Ubungo interchange.
Airport ya kisasa iliyomaliziwa kwa ustadi mkubwa chini ya jpm.
Upanuzi wa bandari ya dar es salaam.
Upatikanaji wa maji kwa zaidi ya 80%.
Ujenzi wa mradi wa mwendokasi mbagala - gerezani.
Masoko ya kisasa kama magomeni, kisutu, tandale na maeneo mengine.
Stendi ya kisasa ya mkoani ambayo ujenzi wake unaendelea.
Machinjio ya kisasa ya vingunguti.
Kituo cha kisasa cha SGR ambacho muundo wa jengo lake unafanana na madini ya tanzanite.
 
Mkuu big up Sana kwa data hoja ujibiwa kwa hoja
 
Mkuu baada ya hii comment,Kama atarudi na huo utopolo wake wa hoja naomba ianzishwe harambee apelekwe hospitali probably atakuwa na corono
 
Mkuu unadhani kujenga soko moja unahitaji kuwa na bei gani? Please zungumzieni issues,umesikia kuwa mkapa alihangaika na hizi petty issues? Sasa nisaidie huo ujenzi wa masoko unasaidieje Tanzania kucompete kwenye regional and global markets?
 
Mkuu unadhani kujenga soko moja unahitaji kuwa na bei gani? Please zungumzieni issues,umesikia kuwa mkapa alihsngaika na hizi petty issues? Sasa nisaidie huo ujenzi wa masoko unasaidieje Tanzania kicompete kwenye regional and global markets?
Kwanza kama umeelewa mainly nimezungumzia ukuaji wa miji ikiwemo jiji la dar es salaam. Huwezi ukaona umuhimu ya barabara kama huna. Hizo advantages zinakuja kupitia ukuaji wa mji.

Huwezi ita petty issues wakati hukuwa nazo na dunia iliyoendelea inazo. Huwezi vutia uwekezaji kama huna hizo unazoita petty issues kama umeme wa uhakika, maji ya uhakika, miundo mbinu ya uhakika.

Ukianza kuzungumzia suala bei utachekesha mzee maana unamaanisha havitakuwa na maana ya kuvifanya sababu ni cheap au?? Je zahanati ya million 400 isijengwe sababu ni cheap?? Unajua umuhimu wa uwepo wa hiyo miradi?
 
Mkapa aligubikwa na rushwa kubwa nyingi. Awamu hii hatujui nn kinaendelea taarifa zote muhimu zimetundikwa
 
Magu hajawahi Jenga barabara Wala kufanya lolote la maana,five years ametembelea nyota ya watangulizi wake huku akitumia propoganda uchwara kuerode akili watu wa aina yako
 
Inawezekana huu ukawa miongoni mwa chambuzi za hovyo 2020! Uchumi hauwezi paa kwa kununua ndege kiholela!
 
Huyo aliyesema kuwa Magufuli aliingia na kukuta reserve ya Taifa $1.8 billion, sijui hizo taarifa anaokototeza wapi!

Mkapa wakati anaondoka aliacha zaidi ya $3 billion. Kikwete aliacha zaidi ya $4.4 billion.

Kati ya Mkapa, Kikwete na Magufuli, katika uchumi Magufuli has performed the worst. Na kwa namna Magufuli alivyoharibu misingi ya ujenzi wa uchumi, hata akipita miaka 5 ijayo yena, hataweza kurekebisha makosa aliyoyayafanya. Katika historia, atabakia kiulinganifu ndiye aliyefanya vibaya katika ujenzi wa uchumi.

Rais aliyefanya radical economic positive changes ni Hayati Benjamin Mkapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utakuwa na minyoo mkuu
 

Machinjio na Stendi ni achievements ndogo sana kwa mtu wa hadhi ya raisi
Ukihesabu stendi zilizojengwa enzi za JK ni nyingi, utakesha, lakini hatuwezi kumsifu kwa vitu kama hivyo.

Huwezi kumsifu rais kwa barabara ya kilometa mbili, ya morocco - Mwenge, tena ambayo mradi ulitafutwa na Serikali ya Kikwete.

sisi tunasifu miradi mikubwa kama
1. Daraja la Mkapa alilojenga BWM
2. Daraja la Kwenye mto Malagarasi alilojenga JK
3. Mradi kama Mwendokasi zilizowekwa na JK
4. Uwanja kama wa Taifa uuliojengwa na Mkapa

Tukianza kusifu vitu vidogovidogo tutakuletea hapa miradi iliyoziduliwa na Mbeba mikasi wa JK Dr Gharib Bilal na tutakesha humu kuiorodhesha. Miradi ua hivyo JK alikuwa haangaiki kuizindua kwa sababu haikuwa hadhi yako

Wewe sifu SGR na Stieglers hayo ni mambo makubwa lakini mambo ya machinjio na Stendi ni vitu vidogo sana kwa hadhi ya rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…