Mookiesbad98
JF-Expert Member
- Feb 1, 2015
- 2,627
- 3,318
Nampongeza sana mh JPM kwa kuvalia njuga suala la Acacia makinikia na hatimaye ungaliwaji na kurekebisha mikataba yote ya madini.
Ni wakati sasa Mh Waziri wa Viwanda na wengine wenye dhamana kuangalia mikataba na kampuni zingine zinavyofanya shughuli zale hapa Tanzania ili nchi pamoja na wafanyakazi wanufaike. Kampuni kama TICTS, Tazara, Nafco na mashamba yao yote kuanzia Hanang,Rujewa-Mbarali,Kapunga madibira, Tancoal,Rubada, Ngorongoro na Tanapa . Tungependa mikataba yake iangaliwe na wahusika washughuliwe inavyostahili. Kama tumeamua kusafisha tusafishe kote. Tiper,Puma energy zamani BP, Sinota na mengine yote tuhakikishe mikataba inanufaisha nchi.
Na tunaomba waziri wa kazi mh Mavunde uangalie pia maslahi ya wafanyakazi. Kuna makampuni ya kichina yanakuja kisanii sanii na kunyima wafanyakazi haki zao. Huu ni wakati wa kusafisha rasilimali zetu.
Heko JPM.