Baa ya Majizo, mgahawa wa Sawasawa tishio kubwa Arusha. Mamlaka ziko wapi?

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
87
280
Baadhi ya baa, lounge na kumbi za starehe Mkoani Arusha zimegeuka kuwa chaka la kufanya vurugu nakuleta kelele kwenye nyumba za watu wanaoishi katika maeneo hayo pamoja na hoteli za kitalii.

Imeelezwa kwamba wamiliki wa kumbi za starehe kama vile acces,The Hub zilizopo maeneo ya Uzunguni Sawasawa iliyopo karibu na hotel ya kibo palace wametoa fedha kwa baadhi ya viongozi ikiwemo NEMC Arusha, Afisa biashara wa jiji, mwanasheria wa jiji, mwenyekiti wa vileo kwa lengo lakuwaruhusu kupiga mziki hadi usiku wa manane,kuendesha kumbi hizo kama night club bila kuwa na leseni jambo linalopelekea kufanya wanavyotaka

Acces inamilikiwa na Majizo ambapo inadaiwa kuwa ana backup Serikalini,The hub inamilikiwa na Kevoo huku Sawasawa ikimilikiwa na dada anayefahamika kwa jina la Agnes ambao wamesema hakuna wa kuwafanya kitu

Wiki mbili zizilizopita kulifanyika ukamataji wa madj na wamiliki wa kumbi hizo ikiwa kama danganya toto kuhalalisha fedha walizopewa huku dc wa Arusha aliyeagiza operation hiyo kufanyika usiku wa manane akikana kuwatuma watu hao.

Wananchi wanaoishi meneo hayo wameitaka Serikali kudhibiti kumbi hizo kwa kuwa wamekuwa hawalali usiku kupitia makelele hayo lakini pia watu wanaofanya biashara hasa mahoteli makubwa na hospitali ya Gemsa AICC na watoa huduma wengine kuingilia kati suala hilo kwa kuwa kila siku kumekuwa na usumbufu wa makelele kupark magari sehemu ambazo hazitakiwa kupiga mziki kwa sauti kubwa na mengine.

Hatukatazi biashara kufanyika ila zifuate sheria kwa kuwa wateja wamekuwa wakikimbia kwenye mahoteli na wagonjwa kushindwa kulala hivyo waziri Mchengerwa anayehusika ikiwemo NEMC fuatilieni suala hili.

.....
IMG-20221123-WA0010.jpg
 
hii nchi taabu sana, kila mahala hakuna control na watumishi wamejitengezea machaka ya kupiga hela kuendeleza maisha binafsi wakisahau wanaoharibikiwa ni ndugu zao.

Wingi wa night clubs bila controlling umefanya hata maadili kwenye jamii kumomonyoka kwa kiasi kikubwa, Umalaya, Ushoga, ulevi kwa vijana umekuwa ni hatari sana sasa hivi.
 
Mbona hii kawaida tu mimi kwangu siku za weekend mziki mpaka alfajiri kwa mbali na ajabu usingizi mtamu mziki kwa mbali ukizima tu mziki na usingizi unakata.
 
hii nchi taabu sana, kila mahala hakuna control na watumishi wamejitengezea machaka ya kupiga hela kuendeleza maisha binafsi wakisahau wanaoharibikiwa ni ndugu zao.

Wingi wa night clubs bila controlling umefanya hata maadili kwenye jamii kumomonyoka kwa kiasi kikubwa, Umalaya, Ushoga, ulevi kwa vijana umekuwa ni hatari sana sasa hivi.
Nilikuwa kwenye kijiwe kimoja ambapo vijana walikuwa wanasimulia kelele za muziki na mambo mengine ya ajabu kwa mila na desturi za Kitanzania hapo coco beach na barabara ya Haile Selassie, Oystebei hususani siku za Ijumaa na Jumamosi.

Ni vigumu kuelewa jinsi watu wanavyopata usingizi wakiwemo watoto. Wenye mamlaka walitazame hili kwa sababu kimsingi makelele hayo na vitendo hivyo ni kero ambayo haiwezi kuhimilika.
 
Hivi huyu wa Sawa sawa village wateja wake wanapaki wapi kwa pale palivyo finyu?
 
Back
Top Bottom