BAA LA NJAA NCHINI: Wananchi Kwimba wamsimamishwa Mkuu wa Mkoa wakiwa na mabua yaliyokauka

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719

Wananchi katika Wilaya ya Kwimba wamelazimika kumsimamisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutokana na tishio la baa la njaa kutokana na mazao kukauka kwa ukosefu wa mvua.

Wakiwa wamemsimamisha Mkuu huyo wa Mkoa huku wakiwa wamebeba mabuwa ya mahindi yaliyokauka, walisema:-

"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, siyo kwamba watu hawajalima, wamelima sana lakini mazao yamekauka kutokana na ukame wa mvua.

Kipindi mvua zikinyesha, ukipita hapa ungeona watu wakitafuna mahindi ya kuchoma barabarani,lakini sasa hatuna namna,mazao yote yamekauka".

Kwa upande wake, RC Mwanza amesema atatuma timu ya Mkoa ili ilishirikiane na Wilaya ili waandae ripoti ya hali halisi iliyopo.

Source: Channel ten.
 
Wananchi katika Wilaya ya Kwimba wamelazimika kumsimamisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutokana na tishio la baa la njaa kutokana na mazao kukauka kwa ukosefu wa mvua.

Wakiwa wamemsimamisha Mkuu huyo wa Mkoa huku wakiwa wamebeba mabuwa ya mahindi yaliyokauka, walisema:-

" Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, siyo kwamba watu hawajalima, wamelima sana lakini mazao yamekauka kutokana na ukame wa mvua.

Kipindi mvua zikinyesha, ukipita hapa ungeona watu wakitafuna mahindi ya kuchoma barabarani,lakini sasa hatuna namna,mazao yote yamekauka".

Kwa upande wake, RC Mwanza amesema,atatuma timu ya Mkoa ili ilishirikiane na Wilaya ili waandae report ya hali halisi iliyopo.

Source: Channel ten.
Huko usukuman atapeleka chakula..tena kwimba alala laaah
 
Yetu macho tu.
Hahahaha sasa kwanini asitangaze wakati ndio ukweli huo.au achune aje atangazr vifo sio.kwa taarifa tuu kenya chakula kipo na ni cheap kuliko tanzania.
mimi nafanyaga biashara ya mahindi mwezi wa sita na wasaba tayari dalili za njaa zilionesha.lakin mtukufu aliruhusu mazao yatoke nje(kosa kubwa)na binafsi nilipinga sana hili.sasa sisi wazalishaji tuna njaa tunaowauzia wameshiba
 
Tanzania mipango na utayari wa kuitekeleza tu ndo tuliporogwa hapo tu. Hata si serikali tu, hata kwetu wananchi.

Mito mingi na maziwa ya maji baridi bado tunalia njaa ni aibu sana. Kuna estates nyingi za miwa ama mikonge au miti, kwanini isifanyike kama ile kwa mazao ya chakula?

Mtu kama Bakresa angewekeza hata kizalendo tu ktk mahindi. Liwe fundisho, mwakani tusimtegemee Mungu wa mvua ktk kilimo kabisa. Huku usukumani jana nusu waue mtu kisa ndiye anaezuia mvua. Ni shida sana.
 
Mahindi gunia 150,000 na unga kilo 1500 kwa kilo toka 1100/1200 na inazidi kupanda lazima namba isomeke kiarabu mwaka huu kama hukuhifadhi na huna hela ya kununua lazima uwe kama mkimbizi..mana Rais ni kama vile hana nia njema na watu wake ..tuliolima mahindi ni muda wa kutengeneza pesa tunauza kwa bei juu bila kuangalia usoni..huku tukiimba "acha muisome namba eeh"..
 
Hahahaha sasa kwanini asitangaze wakati ndio ukweli huo.au achune aje atangazr vifo sio.kwa taarifa tuu kenya chakula kipo na ni cheap kuliko tanzania.
mimi nafanyaga biashara ya mahindi mwezi wa sita na wasaba tayari dalili za njaa zilionesha.lakin mtukufu aliruhusu mazao yatoke nje(kosa kubwa)na binafsi nilipinga sana hili.sasa sisi wazalishaji tuna njaa tunaowauzia wameshiba
Akitangaza asubuhi.....jioni katumbuliwa,akitangaza jioni usiku katumbuliwa..
 
Naamini huyu mkuu wa mkoa hana siku nyingi ofisini.

Kwanin apeleke kwenye media hakumpigia simu.

Anataka kumhujumu kiongozi wa wanyonge eti

Back to the topic

Njaa ipo kwa sababu hakuna mvua katika angle yeyote ya nchi hii.

Hata kama itanyesha inanyesha leo kesho hainyeshi tena.

Kiuhalisia hali ni mbali na hili suala linahitaji kuchukuliwa kwa uzito zaid.

Huku na huku wahisani hawataki kuchangia budget babeki lazima tukae
 
Tegemea kusikia kauli za namna hii kutoka kwa viongozi wa serikali na makada wa CCM.
1/Hao walizoea chakula cha bure
2/Watanzania wengi ni wavivu
3/Kuna watu walizoea dili tu na sasa hakuna dili tena.
4/Hao ni wakulima wanaotaka kumhujumu rais tu
5/Hali ya chakula nchini ni nzuri na chakula kipo cha kutosha na masoko yamejaa nafaka za kutosha.
6/Hizo ni Propaganda dhidi ya serikali ya awamu ya Tano.

HAPA KAZI TU.
 
Back
Top Bottom