Huwa sihitaji hata kulisikia hili jina la huyo jamaa. Umasikini huu tulionao yeye ni anasehemu kubwa ya mchango wake.
Kwa kuwa serikali ya nchi inawajibika kwa wananchi, basi, endapo serikali hii itahujumu maslahi ya pamoja, itakuwa ni haki ya wananchi kuyapinga maamuzi ya serikali au kuivunja serikali hiyo na kusimika serikali mpya, serikali ambayo itawajibika kuzingatia masharti yote, kama ambavyo yatawekwa na wananchi kwa ajili ya kukuza na kuhami maslahi yao ya pamoja.
Mbona naona kama alikuwa amewatega viongozi woooote watakaofuatia baada yake?
Hivi tukijifanya kwamba Azimio la Arusha Bado lipo, na ndio linalotuongoza, hali itakuwaje Jamani?
Nadhani DR SLAA naye alirefer hapa (Kumbuka mahojiano yake na MM)
wewe unafikiri ingekuwa wakati wa mzee kifimbo watu kama slaa wangepona, nyie mchezeeni kikwete tu. wewe unadhani kuna mtu mwingine angeweza kutamka haya maneno zaidi ya yeye nyerere?
nakushauri uache uropokaji maana ukubwa sio umri tu bali na busara zinahitajika, imagine wewe ni askari "kwanza ulishawahi kushuhudia varangati la wakurya wakiwa na rungu?" bunduki yako cha mtoto ukizembea ukapewa moja ya nguvu tunakupa jina jipya. so askari wa tz tuseme wamekua machizi ukiwambia ua wanaua? no! kuna vitu hebu tuchunguzeni kabla ya kuaanza matusiRisasi za moto zimejaa tele vituo vya Polisi, na Askari wetu wamepewa Haki ya Kuua Raia wakati wowote...
Cha Muhimu tuanze kutoa elimu ya Uraia kwa Askari wetu, kila mwana-JF ambaye ana ndugu au Jirani ambaye ni Askari ampe Darasa juu ya Umuhimu wa Raia kudai haki zao kwa njia ya maandamano. Kisha tuwaeleze juu ya Umuhimu wa wao kulinda Raia badala ya kuwafyatulia risasi kwa kufuata maagizo ya wakubwa,, Kisha tuendelee........
Yule Mzee alikuwa na vision ya mbali sana. Hotuba zake nyingi ukizisikiliza bado ziko relevant hata leo hii miaka 26 tangu angàtuke madarakani. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi...AMEN
Kila nikikaa na kupitia azimio la arusha sijaona kosa lake karibu kila kitu ambayo tunashabikia imeandikwa mle.
Sera yetu ilikuwa ya ujamaa na kujitegemea . Nchi hii ni ya wakulima na wafanya kazi. maana neno hii ni kwamba watu wengi ni wakulima na wafanyakazi. Idadi kubwa ya watu wetu ni wakulima wakifuatiwa na wafanyakazi. Hao ndio wenye nchi.
UJAMAA: Ufafanuzi wa neno hili uko hivi uchumi wa taifa ni kwa faida ya watanzania wote. Maana yake ni kwamba kama tunajenga uchumi wetu uwafae watanzania wote. Msimamo huo ukaitwa UJAMAA. Hiyo faida ya wote ndio ikazaa neno UJAMAA. Je uchumi wa tanzania kwa sasa hivi ni kwa faida ya nani? Ebu tusaidiane hapa wajameni uchumi huu unajengwa kwa faida nani kama si ya watanzania wote?
KUJITEGEMEA Tuangalie maana ya neno kujitegemea. Hii ina maana moja tu kwamba kama kweli tunataka kuendelea
ni tujitegemee hakuna njia ya mkato ya kuendelea isipokuwa ni kwa sera ya kujitegemea tu. Huo ndio msingi wa Azimio la arusha . Je leo suala la kujitegemea bado haisitzwi? mbona kila kona watu inawauma kusikia bajeti tegemezi. Sasa kama ndio iko hivyo kwa nini tuliua AZIMIO la Arusha? wakati ilitoa miongozo mingi sana DIRA YA TAIFA, NAMNA YA KUPATA VIONGOZI, MAADILI YA VIONGOZI, MAADILI YA TAIFA, SERA YA UCHUMI NA MISINGI YA UTU.
Naomba tujadili kwa umakini wote suala hili na tutoe solution. kwa upande wangu AZIMIO la Arusha irudishwe.
Kosa kubwa la Azimio la Arusha ilikuwa ni kuwakatia mirija Mabepari wa Ulaya. Sasa hivi wamerudi kwa kasi tena wakisaidiwa na MAKUWADI ambao ni miongoni mwa Viongozi walioko madarakani... Fun facts; Wote waliosoma Harvad University walitekwa na kutumiwa kama Economic hit Men! Mfano mzuri ni Fisadi Andrew Chenge, Ballali, Ndullu, Rostam...wengine ni BWM, Prof Muhongo, Dr Kafumu, Nyalandu, Apson, Mboma, Mgonja et al...
mimi ninachotaka mkuu ni kukirudisha ili tuwe na dira kwa sababu taswira ya taifa ni mbaya sana hakuna hata moja tunaweza kujivunia mambo mazuri tuliyojaribu yameachwa na hatujui tuendako kiukweli kabisa. je unaweza kueleza sera ya taifa letu je ni taifa la ujamaa au ya ubepari. watu wengi hasa wenye nchi hawajui nchi yao inafuata sera ipi?
Mkuu Maganjwa, sera inayofuatwa kwa sasa ni sera ya Uchuuzi mdogo mdogo. wananchi wanaambiwa waunde vikundi ili wapewe mitaji ya kuuza karanga, bamia, kucheza ngoma nk. Viongozi nao wanashindana kuingia mikataba mingi itakayo wapatia vijicent vya kuweka Uswis...
Ni vigumu sana kuirjesha Azimio la Arusha kwa wakati huu; Sera zenye kukinzana tayari tumesha letewa na bunge letu kubariki! Njia kuu za uchumi kumilikiwa na Umma ilifutwa, njia kuu za uchumi zinamilikiwa na akina BWM et al...Tanzania imesha ridhia mikataba feki ya kibiasha za kimataifa, itakuwa vigumu sana kufuta mikataba kama ya dhahabu, uranium, gesi, almasi et al...
Kama nchi tutakachoweza kufanya ni kuweka uwazi katika mikataba na utekelezaji wa bajeti mwanzo mwisho... zaidi ya yote ni kuweka kwenye katiba kuwa adhabu ya Ufisadi ni Kifo na kitekelezwe kwa mtu yeyote hata Rais wa nchi kama walivyofanya Wachina...mwisho na kwa umuhimu: kunahaja ya kureview vipaumbele vyetu ili viwalenge walengwa ambao ni wananchi badala ya kuendelea kuwavutia wanyonyaji...
...Nina matumaini makubwa kuwa hii mikataba ya Wachina inayoingiwa sasa hivi itatusaidia sana kuwabana mataifa ya kimagharibi ambayo huwa wana homola Rasilimali zetu in the name of Jesus na kuwaacha wananchi hoi in the name of shetani...
tuungane shime watanzania AZIMIO la arusha ndio jibu letu
Lirudishwe kama lilivyo KATIKA SURA NA WAKATI TULIONAO ...HAITAKUWA VIBAYA KULIITA AZIMIO JIPYA LA ARUSHA.