Azikwa na Nyoka ndani ya Kaburi lake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Makangaga na maeneo ya Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, juzi walipigwa na butwaa baada ya joka kubwa kutumbukia kaburini wakati mwili wa Mwanawetu Makokola ukiwa umelazwa tayari kwa maziko.

Tukio hilo la aina yake na linalodaiwa la kwanza kutokea kijijini hapo, lilijiri Aprili 8, mwaka huu, saa 10:00 jioni wakati wa maziko wa marehemu huyo.

Hata hivyo, baadhi ya waombolezaji walidai kuwa joka hilo aina ya `jangwa`, halikuleta madhara kwa waombolezaji waliokuwa nje na ndani ya kaburi wakati wakiulaza mwili huo.

Mmoja wa waombolezaji hao, Hamad Issa, alidai kwamba, joka hilo lenye urefu unaokadiriwa mita tano na nusu, lilijilaza pembezoni mwa shimo dogo la kaburi maarufu kama mwana ndani ulimokuwa umehifadhiwa mwili wa marehemu na kutulia tuli bila kuleta bughudha kwa waombolezaji.

Issa aliongeza kuwa baada ya kuliona joka hilo, watu watano waliokuwamo ndani ya kaburi hilo kuulaza mwili wa marehemu Mwanawetu, walikurupuka kutoka nje na kuwaarifu waombolezaji wengine ili waliue na taratibu za maziko ziendelee.

Hata hivyo, alisema baada ya mjadala wa dakika kadhaa, waliamua kuuzika mwili huo pamoja na joka hilo katika kaburi na kurejea nyumbani.
 
Back
Top Bottom