amba.nkya
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 446
- 131
Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar ni miongoni mwa shule za umma (serikali) hapa nchini.
Mkuu wa shule hiyo kwa sasa ni Mwl. Benard Ngoziye ambaye uongozi wake kwa muda mrefu unalalamikiwa na wanafunzi, waalimu,wazazi/walezi na hata waalimu wenzake wa sekondari nyingine kiasi cha kuhatarisha hadhi ya Sekondari hiyo kongwe.
Miongoni mwa malalamiko ya Mkuu huyo wa shule ni kamaifuatavyo:
1. Kuendesha shule hiyo kibabe na kujifanya yeye ni Mungu mtu kwa maana ya kutokuwa na mahusiano mazuri na waalimu na wanafunzi kutokana na kujiamuliwa mambo atakavyo.
2. Kutoitisha vikao vya wazazi na wanafunzi vya kujadili masuala ya shule hiyo kama ambavyo shule nyingine zinavyofanya
3. Kugawa vyumba vya bweni kwa rushwa ikiwa ni pamoja na kuwapa vyumba wanafunzi kutoka nje ya shule hiyo ilhali wanafunzi wake kukosa nafasi shuleni hapo.
4. Wanafunzi kulipishwa michango ya mahafali 20,000/= sawa na ada ya shule kwa mwaka mzima (kutwa)
5. Baadhi ya wanafunzi wamelipishwa michango kama ya vitambulisho, madawati, n.k lakini kwa takribani ni mwaka sasa hawajapata vitu hivyo bila kutolea maelezo.
Hayo ni baadhi tu ya malalamiko dhidi ya Mwl. Benard Ngoziye, Mkuu wa Sekondari ya Azania.
Kutokana na malamiko hayo ndio tunajiuliza Azania Secondari imebinafsishwa kutoka kuwa sekondari ya umma na kuwa mali ya Mkuu huyo wa shule?
Malalamiko hayo yamefanyiwa utafiti na yana ukweli, hivyo mamlaka husika zinapaswa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki kabla ya wanafunzi wakishirikiana na wazazi/walezi wao hawajaamua nini cha kufanya dhidiya udhalimu wa Mkuu huyo wa shule.
Source: Wadau wa Azania Sekondari