Azam watabiri mwisho wa Yanga, Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azam watabiri mwisho wa Yanga, Simba

Discussion in 'Sports' started by MziziMkavu, Jan 17, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  timu ya Azam FC


  Baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi uongozi wa timu ya Azam FC umesema kwamba zama za Simba na Yanga kuongoza soka la Tanzania zimepitwa na wakati na sasa wanaelekeza nguvu zote katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara itakayoanza Jumamosi Januari 21.

  Uongozi huo umesema kuwa kutokana na kuibuka klabu zenye uwezo mkubwa wa kusakata soka, timu hizo zitaondoka katika utawala wa soka hapa nchini kinyume na matarajio ya Watanzania wengi.

  Hayo yameelezwa na Kiongozi Mwandamizi wa Klabu hiyo, Salum Bakharesa katika hafla fupi ya kuipongeza iliyofanyika makao makuu ya klabu ya Malindi Zanzibar hivi karibuni.

  “Moto tulioonyesha katika kombe la Mapinduzi pia utaendelea kuwaka katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara,”alisema Kiongozi huo kuwa timu yake inataka kufikia lengo la kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo tangu kuanzishwa mwaka 2003.

  Bakhresa alisema kuwa timu hiyo imeonyesha kiwango cha hali ya juu katika mashindano hayo na wanamiini kuwa kiwango hicho wataendelea kukionyesha katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

  Hata hivyo alisema kwamba mafanikio yaliyopatikana kwa timu hiyo yametokana na ushirikiano mkubwa waliopata kutoka kwa wanachama na washabiki wa timu hiyo tangu yalipoanza masindano hayo Januari 2 mwaka huu.

  “Kazi kubwa iliyombele yetu ni kuona Azam inafikia malengo yake ya kunyakuwa ubingwa wa soka Tanzania Bara kama ilivyotokea Kombe la Mapinduzi,”alisema Bakharesa.

  Alisema kwamba kitendo cha wapenzi wa timu hiyo kuwa karibu tangu kuanza kwa mashindano hayo kulisaidia kuwapa moyo wachezaji na viongozi na hatimaye kufikia malengo yao.

  Upande wake, Katibu Mkuu wa Malindi, Ali Majjid alisema kwamba ushindi wa Azam wameupokea kama ushindi wa timu yao ya Malindi kutokana na ushirikiano mkubwa uliyopo kati ya klabu hizo.

  Aidha, alisema kwamba siri ya kombe hilo kunyang’anywa Simba imetokan na viongozi wa Azam na Malindi kufanya kazi bega kwa bega tangu kuanza mashindano hayo mwaka huu.

  Timu za Simba na Yanga zilishindwa kumaliza safari ya mashindano ya kuwania kombe la Mapinduzi baada ya kushindwa kuingia hatua ya fainali kwa kutolewa na Azam.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. MUSONI

  MUSONI JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mimi nafikiri hizi ni ndoto za mchana.....kufanikiwa kupata kombe la mapinduzi sio "indicator" ya mafanikio ama kuwa na ule uwanja.kuna vitu vingi katika mpira wa miguu ama mchezo wowote ule....!! hawa sasa naona wanawingu limefunika fikira zao......!!
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hata Birmingham walipata Carling cup mwaka jana na wakashuka daraja.Kombe la mbuzi ni la mbuzi tu.
   
 4. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hao nadhani hawajui fitina za timu zetu hizi kongwe! Nchi hii ni Simba na Yanga tuuuuu! Mimi nawapa miaka miwili ya kuchukua ubingwa wa TZ Bara, baada ya hapo watakuwa ni washiriki tu! Ndani ya timu zote za Tanzania (iwe Bara au Visiwani) kuwa wapenzi wa timu hizi mbili! Siku moja mtayakumbuka maandiko yangu!
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tunaanza na mapinduzi ambalo ni la mbuzi halafu tutakuja na hilo VPL ambalo ni la ng'ombe sawa mkuu..
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Waswahili husema Mdharau mwiba mguu huota tende, Azam itakuwa bingwa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa kwani hizo timu kubwa za Simba na Yanga zilianzia wapi? msije kushangaa kuona Azam Football Club kuwa Bingwa wa Tanzania nzima sio tu tanzania Bara.

  [​IMG]
   
 7. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Labda mwisho wa Yanga, lakini siyo mnyama
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kwa baadae sikatai,ila kudai lazima mwaka huu wachukue mi inanitia shaka.
   
Loading...