Azam Tv wazima matangazo ya bunge live kwa sababu za kiuchwara

structuralist

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,230
907
Katika hali ya kushangaza Azam Extra channel imezima matangazo ya bunge ya moja kwa moja kwa kuwa tu kumeibuka mjadala na mvutano kati ya upande wa upinzani na mwenyekiti wa bunge, Andrew Chenge.

Hali hiyo imesababishwa na wingi wa wabunge kutoka upinzani kuomba muongozo juu ya kutokurushwa live kwa matangazo ya bunge na television ya taifa(TBC)

Ikumbukwe tu hapo asubuhi waziri wa habari michezo sanaa( nape nauye) alitoa hoja ya.serikali kuwa kuanzia jana tbc hawatakuwa wanarushu matangozo yote ya bunge kive.kwa kile kilichodhaniwa ni kupunguzagharama kwani kwa mwaka tbc hutumia 4.2 bilioni kurusha bunge live.

Hata hivyo hoja hiyo ilisababisha ndugu Zito kabwe kuomba muongozo kwakuwa ni haki ya wananchi kupata taari na tbc ni mali ya umma. Hali hii ilipekekea bunge kuahirishwa kwa muda na kamati ya uongozi ilikutana na kulijadili. Hata hivyo jioni hii mwenyekiti wa bunge Andrew chenge ameleza kuwa majadiliano ya hutoba ya raisi yaendelee na kama zito hajaridhika na uamuzi huo basi afuate taratibu zingie. Hali hiyo ndio ilozua mjadala huku wabunge wengi zaidi wakinukuu vifungu vya kanuni za bunge na katiba vilivokiukwa kwa kuruhusu mjadala wa hituba ya raisi kuendelea. Mvutani huo ndio umesababisha azam kukata matangazo yao huku wakisema " kutokana na kile kinachoendela hapa bungeni tunalazimika kukata matangazo yetu"

Sasa najiuliza kwanini wamekata? Kama vunge kuna hoja kinzani nini athari kwao hadi wakate? Kwani wananchi wangeona kungekuwa na nini hasa? Yani nimeshindwa kuwaelewa kama wewe umeelewa tufahamishane.tafadhali.
 
Katika hali ya kushangaza Azam Extra channel imezima matangiza ya bunge ya moja kwa moja kwa kuwa tu kumeibuka mjadala na mvutano kati ya upande wa upinzani.na mwenyekiti wa bunge,Andrew Chenge.

Hali hiyo imesababishwa na wingi wa wabunge kutoka upinzani kuomba muongozo juu ya kutokurushwa live kwa matangazo ya bunge na television ya taifa(TBC)

Ikumbukwe tu hapo asubuhi waziri wa habari michezo sanaa( nape nauye) alitoa hoja ya.serikali kuwa kuanzia jana tbc hawatakuwa wanarushu matangozo yote ya bunge kive.kwa kile kilichodhaniwa ni kupunguzagharama kwani kwa mwaka tbc hutumia 4.2 bilioni kurusha bunge live.

Hata hivyo hoja hiyo ilisababisha ndugu Zito kabwe kuomba muongozo kwakuwa ni haki ya wananchi kupata taari na tbc ni mali ya umma. Hali hii ilipekekea bunge kuahirishwa kwa muda na kamati ya uongozi ilikutana na kulijadili. Hata hivyo jioni hii mwenyekiti wa bunge Andrew chenge ameleza kuwa majadiliano ya hutoba ya raisi yaendelee na kama zito hajaridhika na uamuzi huo basi afuate taratibu zingie. Hali hiyo ndio ilozua mjadala huku wabunge wengi zaidi wakinukuu vifungu vya kanuni za bunge na katiba vilivokiukwa kwa kuruhusu mjadala wa hituba ya raisi kuendelea. Mvutani huo ndio umesababisha azam kukata matangazo yao huku wakisema " kutokana na kile kinachoendela hapa bungeni tunalazimika kukata matangazo yetu"

Sasa najiuliza kwanini wamekata? Kama vunge kuna hoja kinzani nini athari kwao hadi wakate? Kwani wananchi wangeona kungekuwa na nini hasa? Yani nimeshindwa kuwaelewa kama wewe umeelewa tufahamishane.tafadhali.

Azam TV nayo ya KODI ZENU?
 
Bunge la sasa ni la kibabe hakna tena uhuru wa vyombo vya habari, na pslee wamekata ili wananchi wasione aibu iipatayo serikali
 
Wamekata kwa sababu lengo sio TBC wasionyeshe bali watanzania hawatakiwi kuona kinachotokea bungeni live. Walisahau kuwa TV binafsi zimo na ndo Nape akaja na hoja ya gharama. Wamestuka Azam wanaonyesha imebidi wapigwe mkwara wazime matangazo ndo maana wamekata
 
Nimefatilia mjadala mzima, kwanza nawapongeza azam media kwa kuona umhimu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge la 11 pasipo kuogopa gharama. Hidhana ya kupunguza gharama imechuliwa vibaya na baadhi ya watendaji wa serikali,Kwa hili la TBC lazima serikali ikubali kuingia gharama ili wa tanzania tupate haki yetu ya kikatiba ya kupata habari. Kuhusu azam kukatisha matangazo nadhani ni maadili ya kazi.
 
sasa kama tbc 1 wanapata hasara inakuwaje tena azam wamezima hayo matangazo wakati kwa azam ndio vizuri ili wauze vingamuze vyao kwa wingi ili walipe kodi nyingi
 
Back
Top Bottom