Mungu hebu tukumbuke wa watanzania, tumechoka kudanganywa km watoto, tumechoka kutukanwa Na kudhalilishwa kwa kuitwa wapumbavu Na malofa, kila Leo hali inazidi kuwa mbaya, Ee Mungu uishiye inatosha sasa kwa ufedhuli huu tunaofanyiwa,
Ee Mungu Muumba mbingu Na dunia, wananchi wa Tanzania, tunakushtakia wewe kwani ndiwe hakimu wa mwisho, hukumu hawa watu, wAmetudhalilisha sana, wametuonea sana, na kututukana sana, wananchi tumechoka.
Mungu, maombi yetu ni dhaifu Na hayatoshi kitu kwako, lkn Km wazalendo Na wenye uchungu Na nchi yetu, tumechoka kwa kuugua maana kila usiku twalia, tunalowesha magodoro yetu kwa machozi, tunaomba utujibu, usikawie, tumekauka Na ni dhaifu uko wapi Mungu wetu?