Azam Tv vifurushi vyenu havina mvuto, burudani kwa wote imeenda wapi?

anaesthetist

Member
Mar 20, 2016
27
22
Pamoja ya kwamba mmetulazimisha kuongeza bei ya vifurushi kwa kutulazimisha tuongeze Tshs 3000/= kwa vifurushi ambavyo wala sio wote tunaovipenda, mmetuboa watu wengi sana. Mlikuja kwa mkwara sana ila naona kama mnaanza uswahili.

Nakubali kuwa nyie ndio viongozi wa kuleta manadiliko ktk tasnia hii ya Tv kwa hapa Tz.

Sasa hivi kifurushi chenu cha chini ni Tsh 15000/=, hii kwa mtanzania wa kawaida ni nyingi sana. Ongezeko la Tshs 3000 pia litawaweka wengi pembeni waliokuwa wanajikongoja na kifurushi cha awali cha Tshs 12000/=.
Mngeacha kile kifurushi cha Tshs 12000/=, na kuwa pia na hiki cha Tshs 15000/=, wana sports ambao wangekitaka hiki cha sasa wangekinunua ila sio kutulazimisha wote. Kwa wanamichezo ni furaha tupu sasa hivi, Je sisi tusio wanamichezo wa soka inakuaje? Binafsi naona mngekiacha kile kifurushi cha awali cha bei ya chini au kama mmetulazim tuongeze bei basi angalau mngeongeza chanel kama BBC na NatGeo na Discovery ktk hiki kifurushi kipya cha bei ya chini.
Nimebaki najiuliza hii burudani kwa wote mna maana gani?
Mnapopanga vifurushi muwe mnatushirikisha sisi wadau, sio mnavipanga mtakavyo nyie.

Timizeni kauli mbiu yenu ya burudani kwa wote.
 
Back
Top Bottom