mangonjoli
Senior Member
- Aug 29, 2012
- 154
- 110
Nimekuwa nikiufatilia ujinga wa Azam TV kwa muda mrefu lkn leo imenibidi nije niongee pumba zao zinazotufanya Watazamaji tukose hamu yakuangalia Movies zao. Wamefanya jambo zuri kuingiza sauti za kiswahili katika film zao wanazotuonyesha lkn Tatizo kubwa walionalo ni kuingiza sauti za makabila mbalimbali kama Wachaga, Wapemba, Wahaya na hata wasambaa katika Movie za kihindi na hata za Kizungu.
Unakuta muhusika muhindi kwenye film anaongea kipemba au kizigua hii inaharibu kabisa ladha ya movie na lile kubwa walilolifanya la kuzitafsiri kupoteza ladha.
Kuna siku walionyesha movie moja ya kijeshi ya wamarekani nilipigwa na butwaa eti Star kwenye ile movie anamwambia mwenzie wawahi kwenye kambi yao LUGALO wakakamilishe mipango. Nilizima Tv hapohapo.